Posts

📕TAMBUA HATUA KUU 5 ZA MAHUSIANO HADI NDOA💍🤵🏾‍♂️👰🏾

​ Ziko hatua 5️⃣ za kupitia unapoingia kwenye mahusiano hadi ndoa, na hatua hizi ni jambo la msingi sana kwanza kuzitambua na kisha kuzipitia. 👌🏾 Hatua hizi zisipofuatwa kwa ukamilifu moja ya madhara yake ni mahusiano kuvunjika 💔na moja ya hatua hizo ambayo sasa hivi inarukwa sana ni hatua ya uchumba mahala pa kuboreshana na kuonyeshana tabia za asili. Bahati mbaya mahusiano mengi hayana hatua hii, watu wanaoana wakiwa bado kwenye hatua ya wapenzi hivyo wakifika ndani ya ndoa, gomvi ni nyingi sababu wote hawakujiandaa na tabia za asili za mwenza wake. Ni jambo la msingi kuzitambua, ndani ya kitabu hiki nimekuandikia hatua zote kwa utuo na maelezo zaidi ili uelewe ni wapi hasa panapokuangusha na hatua gani ilirukwa ama mahusiano yako yako hatua gani kisha ujifunze maana ya kila hatua ili ipite kwe kuelewa sio kwa kukisia. 📕Kitabu kinapatikana katika nakala aina mbili,  🗣️nakala ya sauti - Tshs 25000 na  📕nakala ngumu - Tshs 20,000  Ili kukipata kitabu hiki fuata link...

TAMBUA : BIASHARA NI RAHISI KUIFANYA KWA KUFIKIRI ZAIDI YA UHALISIA WAKE

Image
Wapo watu wengi waliofeli kwa changamoto ya kuifanya biashara kwa kichwa zaidi ya uhalisia wake, yako mambo mengi ya kufahamu kuhusu biashara lakini la kwanza katika yote ni kutambua uhalisia wa biashara kwa kuwa na taarifa sahihi na sio maelelzo ya kufikirika. UTAFELI VIBAYA kwa kutegemea taarifa za kufikirika. Niambie ulijaribu biashara gani kwa kufikiri na uhalisia wake ukakukataa? Ikiwa unahitaji ushauri ama usimamizi bora wa biashara yako wasiliana nami sasa : 0745 108010 ——————————- Mahusiano ndio msingi mama wa mafanikio yetu kila linalofanyika liko chini ya kiwango sahihi cha mahusiano, unaifahamu Saikolojia ya Mahusiano?, Kama bado tayari nimekuandikia kitabu ambacho kitakuongoza kujenga ufahamu chanya wa nini maana na saikolojia ya mahusiano kwako na kizazi chako. Jipatie leo nakala yako kwa Tshs 20,000/= nakala ngumu na Tshs. 25000/= nakala ya sauti. Kukipata wasiliana nami leo  0745108010 #echumaarifa #ujasiriamali #maisha #daressalaam #elishachuma

JENGA MAZOEA YA KUANDIKA MAWAZO YAKO.

Image
Akili zetu zimeumbwa kuwa na maboresho ya mawazo kulingana na msimu ama uhitaji husika, hii imekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana wanapofikiria kuanzisha ama kukamilisha malengo yao, wanapoanza wazo linakuwa jingine na wanapoendelea pia wazo linakuwa jingine hii inapelekea kupoteza nguvu katika kusimamia misingi ya wazo la kwanza. Sasa basi jitahidi sana uwe unaandika mawazo yako ili unapoyafanyia kazi uwe na sehemu ya kumbukumbu ambayo utaitumia kwa ajili ya kukuongoza katika yale ambayo unafikiria kuyafanya, kuandika inaweza kuonekana kama ni kitu kidogo sana katika utendaji lakini ni kitu kikubwa sana kisaikolojia na pia hata kimalengo. Nijulishe hapa chini, na wewe ni mtu wa kuandika malengo yako au unakiamini kichwa chako kwamba siku zote utakumbuka na kulisimamia lengo mama. Bado kitabu cha Saikolojia ya mahusiano kinapatikana, ni kitabu maalum kwa ajili ya kuinua na kurudisha uelewa bora wa mahusiano kuanzia yale ya mzazi na mtoto hadi yale ya kimapenzi, saikolojia yake isip...

Matumizi sahihi ya elimu yako.

Image
Kwanza kabisa ni jambo la msingi kutambua na kuiondoa dhana ya kuwa mjinga ni tusi,ama kushushwa hadhi HAPANA. Mjinga ni mtu asiekuwa na uelewa wa kitu ama jambo fulani,hivyo ifike mahala izoeleke tu kuwa wewe ni mjinga wa kitu fulani  na isiwe ni tusi ama udharirishaji kwako. Lakini dhima ya bandiko hili iko kwenye muktadha wa matumizi ya elimu zetu kwa manufaa ya baadae,tumepita kwenye kipindi ambacho dhana kuu ya elimu ilikuwa ni kusema umesoma chuo ama sehemu fulani na uko na vyeti vingi,kipindi hiki kimetuathiri kwa kiasi fulani kwani kimetengeneza wahitimu wengi wenye vyeti lakini hawana uwezo sokoni. Lilipokuwa tatizo tena wakaanza kulalamika wazee wameshikilia nafasi za ajira zao hivyo hawawezi kuajiriwa, lakini swali ambalo hawakujiuliza ni kwanini hadi leo bado hawana kazi lakini wana elimu, na Je ni kweli kuwa bila kuajiriwa elimu yako haina kazi?. Watu wengi tunajisahau sana na kuacha kutumia elimu ila tunakimbilia makaratasi,mabadiliko ya kipato yanaanza na mbadiliko y...

Kutunza ni kuchelewesha matumizi

Image

Jiandae kufeli

Image
Biashara,Mahusiano,Mipango mingi inafeli sababu watu hawajiandai na changamoto za anachokitafuta ama kukifanya matokeo yake anawaza faida tu,zinapokuja changamoto zake anajikuta anafeli kirahisi sana Biashara nyingi zinapoandaliwa huwa ni kw mpango wa "high season" mauzo yako juu lakini uhalisia hakuna biashara ambayo inakuwa kwenye high season mwaka mzima ni lazima kuwe na kipindi cha "low season" mauzo hafifu na hapo ndio biashara nyingi hufa,kwa kuwa hazikujiandaa na low season matokeo yake ni kula mtaji na kupumzika,hili ni janga la biashara nyingi...UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WAZA NA KIPINDI CHA KUFELI AMA KUPOROMOKA KWA BIASHARA UTAFANYA NINI?. Kwenye mahusiano wapenzi wengi huingia wakitegemea raha tu na furaha na mara nyingi mwanzo wa mahusiano kila mtu hujitahidi kufanya ili kumridhisha mwenzake,ila baada ya muda ile hali ya kuridhishana huisha huingia hali ya uhalisia hapo ndio shida huanza,vikwazo,wivu,husda,vijitabia huonekana,sasa kwa kuwa akili ya weng...

Mafanikio na gharama zake.

Image
Nimekuwa nikikutana na kujadiliana na watu wengi sana kuhusu mbinu na jinsi ya kufanikiwa,nimegundua watu wengi wanayapenda sana mafanikio na wanatamani kufanikiwa lakini hawakotayari kuzibeba gharama za mafanikio hayo. Kufinikiwa ni kupiga hatua na hakuna hatua inayopigwa bila kutumia nguvu,hata hatua ya mguu wako ili unyanyuke unahitaji nguvu,balance,uelekeo na mambo kadha iko hivyo pia kwenye mafanikio. Ili ufanikiwe lazima uzikubali gharama za eneo lako la mafanikio,usiwe kwenye kundi la kutamani kila siku na ku"wish" jitoe kwenye hiyo hali kwa kubadilisha mawazo yako. Na ili ufanikiwe utakavyo tumia gharama kutengeneza mafanikio yako,usiombe kila kitu wakati wewe unatengenezewa kitu. Mafanikio yanaanza na mabadiliko ya tabia na mtazamo,anza kufanikiwa ndani yako sasa ili uyatengeneze mafanikio ya nje. Elisha Chuma. Mwalimu,Mshauri & Kocha wa Mafanikio