Posts

Showing posts with the label wazo la biashara

Elisha Chuma: Simamia wazo kuu

Wengi huwa tunakimbia wazo mama na kukimbilia mawazo mtambuka bila kukumbuka bila wazo mama mtambuka lisingeonekana. Simamia wazo kuu,unapelitenda wazo mtambuka hakikisha wazo kuu haliathiriwi. Elisha Chuma +255 745108010

Wazo la 3

Vijana wengi na watu wengi wamekuwa na shida ya ajira sasa hivi ambapo imefikia hatua inabidi aajiriwe katika sekta isiyokuwa na weledi wake na wengine kukosa kabisa,wengine wanapesa za mitaji lakini hawana wazo bora la biashara waanzishe kitu gani ili kiwe na mafanikio kwao. Leo hii tutaenda kuangalia wazo jingine la biashara ambalo litawahusu sana akina mama na akina dada,katika mzunguko wa maisha wote tunatakiwa kutambua Mungu ni kiongozi na katika uumbaji wake hakuna alieumbwa kwa bahati mbaya na ndani ya kila mtu kuna kitu cha ziada ambacho Mungu amemuwekea kulingana na utashi wake..Leo nitawapa mbinu ya kujiajiri kwa madada ambao wanasema hawana ajira kabisa. Kuna baadhi ya kazi ambazo kama mdada ama mwanamke ukifanya kwa uhakika zinakutoa na hazihitaji chuo wala cheti ni kipaji na baraka tu baadhi ya kazi hizo ni pamoja na ususi,kutengeneza vitafunwa(bites),kufanya usafi na kadhalika,kama wewe unajijua unakitu unachoweza kukifanya kwa ufasaha kwa moyo wote bila kushurti...

Wazo la biashara 01

Asilimia 80% ya dawa tunazotumia mahospitalini zinatokana na miti,na asilimia 60 ya magonjwa tunayougua yanatokana na mtindo wa maisha, hivyo ukiwa kama mjasiriamali ama mfanyabiashara unatakiwa uone fursa hapo katikati ya kuugua na miti. Matunda yanatumika sana kama dawa, na chakula ni dawa ndio maana ukikikosea kinakuwa sumu mwilini sasa tupitie fursa hii,ikakufungue na kukupa maono mapya. FURSA: Unaweza  kuuza ujuzi  ama kuwa mshauri wa masuala ya chakula,matunda na miti. JINSI YA KUIFANYA: Kama mtumiaji wa mtandao anza kwa kutafuta na soma kwa makini    matumizi,faida,utengenezwaji,uhifadhi na mfumo wa mwanadamu unavyopokea na unatumia nini kwa matunda ambayo yanapatikana sana eneo lako ama yanayopatikana kwa urahisi ( Mfano kuchanganya tunda lenye ukali na lisilokuwa na ukali unaliua lile tunda lisilokuwa na ukali linakuwa pombe(Nanasi na ndizi).),fuatilia na chakula uandaaji,viungo,upishi na kadha wa kadha hakikisha unatambua kila aina ya chakula tunda ...