Posts

Showing posts from August, 2013

Maana ya Branding kwa mfanyabiashara na Mjasiriamali

                                           Maana ya branding kwa mfanyabiashara Branding ni muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemtarajia   kwa maana hiyo brand Inahusika na inanafasi kubwa katika ukuzaji wa biashara yako na   maendeleo yake kila   jina ni Brand lakini sio kila brand ni jina hivyo ili jina liwe brand linahitaji   vitu fulani fulani ili kuwa hivyo Mfano: Naseeb Abdul ni jina lakini Diamond ni brand. Ikiwa inamaana ya kwamba ili uwe na kitu au Uonekane katika kipengele au sehemu yako ya ushindani ni lazima uwe na brand na sio jina.Ukiwa kama mfanyabiashara ambaye unafanya biashara sio kwa majaribio brand ni lazima katika  biashara yako , Brand inatakiwa kuanza kutengenezwa tangia mwanzo wa biashara   ili kuipa nguv...

Matumizi ya blogu hii

Blogu hii ni kwa ajili ya kukuza na kuelimisha kuhusu biashara na ujasiliamali blogu hii inasimamiwa na kuendeshwa na Elisha Chuma mwenyewe . Kwa wenye maswali yoyote kuhusiana na biashara , ujasiliamali au kitu chochote ambacho kiko katika mzunguko wa branding,biashara na ujasiliamali unakaribishwa sana. Jinsi ya kushikiriki fungua user name yako na weka swali lako au maoni yako kwenye post itakayokuwepo juu au tuma swali lako kupitia elishachuma@gmail.com na nitalitoa na kuliandikia majibu yake haraka iwezekanavyo kulingana na idadi ya maswali. Asanteni sana na karibu katika ulimwengu wa kuelimishana Elisha Chuma

Tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali (Jitambue)

Tofauti kati ya ujasiriamali na ufanyabiashara Ujasiriamali unaweza kuipata maana yake halisi kwenye Jina lenyewe ujasiriamali ( ujasiri kwenye mali) hivyo ili Kuwa mjasiriamali lazima uwe jasili na   mwenye uwezo Wa kukubali matatizo na changamoto, uwe tayari kupoteza Sasa hivi kwa ajili ya mafanikio ya baadae. Ukiwa mjasiriamali faida za muda mfupi kwako huwa sio za muhimu sana na lengo Kubwa huwa ni kufikia malengo uliyoyapanga na kukamilisha ulichokifikiria Watu wengi hujiona ni wajasiriamali kwa vile tu huwa na uwezo wa kutatua matatizo Ya biashara yake kwa kutumia njia nyingine . Mfano: utakuta mtu anafanya kazi ameamua kuanzisha biashara yake pembeni ya kazi Anayoifanya ambapo inafikia hatua anapata hasara au bashara hailipi kwa muda husika Anachoamua kufanya ni anachukua fedha kutoka sehemu anakofanyia kazi anaziba pengo Lililopo kisha anaendelea na biashara, huyu anaweza kujiona ni mjasiriamali lakini sio Huyu ni mfanyabiashara ....

vitu vya kutambua baada ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

biashara au ujasiriamali ni ndoto za watu wengi lakini asilimia kubwa husahau vikwazo na vizingiti ambavyo hutokea kabla na baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara  toleo lililopita nilielezea vitu unavyotakiwa kufanya kabla ya kuwa mjasiriamali, leo nitaelezea vitu unavyotakiwa kuvifanya baada ya kuwa mjasiriamali . kuna vitu na mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafata ili ufanikiwe katika kila hatua ya biashara au ujasiriamali wako baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na                                     Baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara                           1. Biashara ni ushindani, na nafasi ya makosa   Moja kati ya vitu ambavyo unatakiwa k...

Vitu vya kutambua kabla ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

Vitu   vya kutambua kabla  ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali   Ujasiriamali  imekuwa ni ndoto ya watu wengi sasa hivi, kila anaepata nafasi au wazo la biashara huanza kujiita mjasiriamali lakini kuna maana na mambo mengi ambayo mtu anatakiwa ayajue kabla ya kuanza biashara na anatakiwa achague kati ya ujasiriamali au ufanyabiashara. leo nitaelezea mambo kadhaa ambayo unatakiwa kuyafahamu kabla ya kuwa aidha mjasiriamali au mfanyabiashara na baadhi ni mambo ya kawaida na tunakutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku lakini ni sawa na ukiona sululu bila kuambiwa ni sululu na inafanya kazi gani utakuwa unaona iko kama uma lakini unaweza kupatia  au kukosea matumizi yake kwa kuiona tu, vivyo hivyo hata kwenye ujasiriamali pia kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifahamu.unaweza kuvifanya bila kuambiwa na ukawa sawa ila ukiambiwa utaweza kujiamini na unachokifanya zaidi ya mwanzo. Kabla ya kuanza biashara 1. Kukubaliana na hali   ...

Vitu vya kuzingatia unapofanya Branding

Kuna vitu vitatu ambayo hutumika sambamba   ili kutengeneza 244  yenye afya Logo - Nembo Nembo   ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako Branding- kulijengea jina utambulisho Branding ni kutengeneza uaminifu na ahadi ya bidhaa yako kwenye akili ya mteja unaemtegemea Ambapo brand huunganishwa na bidhaa kwa mteja . Identity - utambulisho ( marketing,advertising,publication,sales) Hii inamaanisha aina ya utambulisho utakaotumia kujitambulisha, unaweza kujitambulisha kama expert Kujitambulisha kama mzoefu kujitambulisha kwa aina ambayo wewe itakupa ahueni na upenyo kwenye soko ulilopo

Maswali 12 kuhusu Branding

Maswali ya Msingi unayotakiwa kuyafahamu kabla ya kuanza kubrand. 1. Brand ni nini? Brand kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni muonekano wako Kuhusu biashara yako na jinsi gani biashara yako inajitofautisha na washindani wenzako, 2. Kazi za Brand. Brand hutambulisha muonekano ,ubora wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic(kawaida) hazijulikani na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu. Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji. Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa. 3. Kwanini ufanye brand     Unafanya brand kwa sababu unataka kutambulika na kuongeza mauzo , pia ni kutaka     kujitofautisha na washindani wako 4. Faida gani unayoipata uk...