Elimu inayokosekana
Elimu inayokosekana na inayowapoteza wengi katika maisha Katika mfumo wetu wa elimu kuna elimu muhimu inayokosekana na hakuna sehemu ya kuipata hadi Ujitambue mwenyewe ambapo elimu hiyo ni elimu ya kujitambua, Tatizo lililopo katika elimu yetu ni kwamba tunasoma kwa kufuata taratibu za watu fulani, mfumo wa elimu tunaotumia Ni wa mzungu , ili ujikomboe unatakiwa ujitambue, mzungu alileta elimu lakini haikuwa elimu ya kutufanya tujitegemee Elimu tunayoipata kwenye shule zetu kuanzia ngazi ya chekechea hadi ngazi ya sekondari ni elimu ya lugha na kusoma na kuandika, kama ni hivyo kwa nini basi tuendelee kupoteza muda wingi kusumbukia kusoma na kuandika?. Wanafunzi wanachukua hadi masomo 14 yote ayafanyie mtihani na anatakiwa kufaulu ni uwezo wa hali ya juu unaotumika kwa wanafunzi wanaofaulu, na hicho hakikuwa kizazi cha dot.com ambacho kila kitu wanafunzi wanatumia Mbadala wa google kutafuta.hata kufeli sana kwa wanafunzi wetu kumesababishwa na mabad...