Posts

Showing posts from October, 2013

Tahadhari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali

Taa ya hatari imeanza   kuwaka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Tanzania Asilimia kubwa ya wafanyabiashara, ( wakubwa na wadogo) wanafanya biashara Kienyeji na kikubahatisha wanafanya biashara kama mchezo wa bahati nasibu kupata Kukosa   lakini siku sio nyingi mambo na hali itabadilika na kubadili mfumo wote wa kibiashara Hapa Tanzania. Kwa kuanza kwa sasa watanzaia wengi wanapata hamasa na hamu ya kuwa wafanyabiashara Au wajasiriamali kwa inspiration kutoka nchi za nje, kutoka kwa wajasiriamali wakubwa , kutoka Kutoka katika vitabu vya waandishi wa nje ambao huelezea hali ya biashara au ujasiriamali kwa Kiwango na uwezo wa sehemu walipo na kwa mjasiriamali   wa kawaida akisoma au kutumi mbinu zile Zinaweza msaidia sababu kwa kipindi hicho vitu alivyovisoma sehemu anakovitumia havijulikani hivyo Hata akikosea au kipatia hakuna atakaetambua,hiyo ndiyo hali iliyokuwepo kwa Tanzania ya zamani lakini Kwa sasa hali inabadilika tena sana . ...

Vitu vitano vinavyosimamia biashara yako

Biashara pia inavitu ambavyo kila mtu anatakiwa avifuatilie ili uweze kuimanage, biashara nyingi zinafeli   iwapo moja kati ya vitu hivyo vinapopungua au kukosekana hivyo basi kabla ya kuanzisha au kuanza biashara yako jiaminishe unaweza kusimamia vitu vifuatavyo. 1.Branding Branding ni muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemkusudia, hii ikiwa inamaanisha lazima ujue mteja wako anataka akuonea katika hali gani ili akuamini , mteja wako unataka apate kitu gani kichwani mwake mara tu akiiona alama yako nakadhalika,kuijua elimu hii kutakusaidia sana katika uendeshaji wa biashara yako kwa sababu itakuwa ni rahisi kwako kujua saikolojia ya mteja wako na kuepusha kufanya yasiyo sawa katika biashara   na pia ukiiifahamu branding itakufundisha pia   njia za   kupambana na wateja na mbinu za kiushindani. 2.Masoko ( Marketing) Masoko ni sehemu ambayo inahitaji umakini mkubwa baada ya kufanya brand ya biashara yako kitu kinachofuata ni kutengeneza na kutafuta...

Makosa yanayofanywa na wanaotoa elimu ya ujasiriamali

Kuna kitu ambacho wananchi wanakuwa wanapotea bila kujua kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaohamasisha na kutoa elimu kuhusu ujasiriamali, Sio wote Watu hao wanawasaidia watu,lakini wanaruka sehemu kubwa ambayo inawaumiza sana Watu wanaoamua kutumia elimu yao kwa manufaa yao,mfano kuna wale wanaotoa elimu kuhusu Kutengeneza vitu kama sabuni,shampoo na vinginevyo,hao hutoa tangazo la kuwafundisha watu mbinu Za kuwa mjasiriamali, wao hufundisha namna ya kutengeneza hadi unaelewa halafu wanakuacha.hilo Ni kosa kubwa sana kwa wao kumfundisha mtu kutengeneza kitu kinachofanywa na makampuni makubwa kama kazi yao halafu ukamfundisha yeye kwa shilingi elfu 30, bila kujua atatoka hapo atatafuta fedha ya mtaji na mtaji wa kwanza unaweza kuwa ni 50,000 tu hapo ameshapigia hesabu akiuza anauhakika wa kutengeneza fedha nyingi halafu inakuwa tofauti. Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaoitwa walimu wa ujasiriamali   wanaofundisha mbinu za ujasiriamali siwapingi wala sikidhan...