Hatua za kufuata unapofikiria kuanza ujasiriamali
Ujasiriamali sio kitu kidogo kama wengi wanavyofikiria na wengi hufikiria kupokea hasara ni kama vile umefungua duka hujauza vitu hadi muda wake wa kutumika umeisha ndio unakuwa umepata hasara lakini kwa maana ya ujasiriamali maana iko tofauti kidogo maana ya kukubali hasara kwa upande wa ujasiriamali ni ile hali ya kukubali kutumia nguvu na gharama nyingi kwa ajili ya matokeo ya baadae ,ambapo matokeo hayo yanaweza kuchukua muda mrefu hadi yaonekane. Mjasiriamali ni mfanyabiashara pia na hakuna mfanyabiashara anaefanya biashara kwa hasara kila kinachofanyika katika biashara kinategemewa kulipa hata kama sio sasa, hivyo hata mjasiriamali pia hakubali hasara ila kwa malengo. Hivyo unapoamua kuwa mjasiriamali usikurupuke kwa vile unajiona unaweza kwanza kabla ya yote jitambue kwanza (tofauti kati ya ujasiriamali na biashara),ukishakuwa na uhakika na hilo sasa unaweza kuanza kufata hatua zifuatazo,nb: usifanye kwa kuwa unataka kujilazimisha kuwa mjasiriamali fany...