Posts

Showing posts from December, 2013

Aina za washindani katika biashara

Katika kila biashara lazima kuwe na washindani, biashara isiyokuwa na washindani hiyo sio biashara   na katika biashara Ushindani ni wa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya biashara yoyote na   moja kati ya faida za washindani ni kuongeza changamoto za ufanisi wa kazi,kuna aina kuu   tatu za washindani Washindani wa moja kwa moja Hawa ni washindani ambao unawafahamu na mnashabihiana biashara,mnafanya biashara ya aina moja,kwa mfano kama biashara yako ni fundi cherehani basi mafundi cherehani   wengine ndio washindani wako wa moja kwa moja. Washindani wasiokuwa wa moja kwa moja Hawa ni washindani ambao wanatengeneza bidhaa au shughuli mbadala ya za kwako, wanatengeneza   aina ya bidhaa ambazo kama mteja asipotumia za kwako basi atatumia za kwao. Mfano: kama wewe ni fundi cherehani washindani wako ambao sio wa moja kwa moja ni wale ambao wanauza nguo madukani za spesho na mitumba hao ni washindani wako pia. Washindani dhahania Hawa ni a...