Posts

Showing posts from February, 2014

Semina

Elisha Chuma   ameandaa mpango kabambe wa ushauri wa biashara kwa wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa na wale wanaotaka kuanzisha biashara ili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa na wenye mafanikio. Mtu atakakayejiunga na mpango huu atapewa mbinu za hali ya juu za biashara na uwekezaji ambazo zitamuwezesha kuinuka kiuchumi na kuwa mfanyabiashara mkubwa kwa haraka. Mtu yeyote anaweza kujiunga na mpango huu ambao mkataba wake utakuwa ni wa mwaka mmoja mmoja ambao unaweza kurudiwa tena.Kwa nini Elisha? Elimu ya biashara anayoitoa haipatikani sana hapa nchini japo mfumo wake wengi wanautumia. Kitabu chake cha Siri za kushinda katika biashara kupitia branding, kimewainua wajasiriamali wengi . Manufaa ya kujiunga na mpango huu; Utapewa mbinu za hali ya juu za biashara na uwekezaji ambazo zitakuwezesha kuinuka kiuchumi na kuwa mfanyabiashara mkubwa kwa haraka. Utajiunga na mafunzo maalum ya ujasiriamali kwa email kipindi chote utakachokuwa umelipia michango....

Jinsi ya kutengeneza mpango biashara ( Business plan)

Katika dunia ya sasa utengenezaji wa   mpango wa biashara umekuwa ni lazima na kwa biashara yoyote unayoifanya bila kuitengenezea mipango haiwezi kufanikiwa, leo nimeamua kuanza na baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuyafahamu unapotaka kutengeneza mpango wa biashara . Hapa chini vifuatavyo ni vitu muhimu unavyotakiwa kuvizingatia katika utengenezaji wa mpango biashara wako, andika kwa umakini kiini cha wazo lako la biashara na lijumuishe   vitu kama. 1/ Jina 2/ Aina ya biashara 3/ Historia ya biashara na maendeleo   yake 4/ Huduma /bidhaa 5/   Tathmini   ya Soko 6/ Ushindani 7/ Masoko 8./Ufanyaji kazi 9/ Usimamizi na utawala 10/ Uwezo wa wafanyakazi 11/Matatizo na utatuzi 12/ Maelezo ya kifedha Jina na aina ya biashara Kipengele cha kwanza na cha pili ni kama vinashabihiana kwanza ni inatakiwa uandike jina la biashara unayotegemea kufanya ( hapa sio aina ya biashara) ni jina linalokutambulisha wewe katika biashara , Pia hapa ...