Kumekuwa na Mkanganyiko wa matumizi pia ya hivi vitu viwili Branding na Marketing ( Masoko) na imekuwa ni tatizo kugundulika ipi inayotakiwa ianze kati na ipi ni kubwa zaidi ya mwenzake . kwa upande wa Branding tayari nilikwisha elezea kwenye toleo za nyuma Branding . Leo nitaelezea kidogo maana ya masoko na tofauti yake na Branding Masoko (Marketing) ni kila mkutaniko wa kampuni yako na mtu au kitu chochote duniani Maana ya marketing ( Masoko) inajumuisha; Jina la biashara,mgawanyo wa aidha unatoa huduma au bidhaa,njia za utengenezaji au utoaji huduma,rangi,saizi na umbo la bidhaa yako,upakiaji,eneo la biashara,kujitangaza,mahusiano na jamii, tovuti,Branding,email,sahihi yako kwenye majarida na chochote unachokitoa ,ujumbe wa sauti,matamasha ya mauzo,simu,mafunzo ya uuzaji,jinsi ya kutatua matatizo, mipango endelevu ,watu wanaokuwakilisha,wewe,unavyofuatilia Lakini pia kwa upande mwingine marketing(Masoko) inajumuisha,wazo kuu la brand yako,huduma yak...