Aina tatu za imani zitakazokurudisha nyuma katika biashara yako
Biashara haiangalii unaamini kupitia nini, biashara haiangalii wewe ni mkristo,mpagani muislamu au mhindu,lakini kuna imani ambazo biashara inakutengenezea na inataka ufanikiwe kupitia hizo, hivyo ilikufanikiwa katika biashara yako unatakiwa upitie ukipishana nazo lazima matokeo yake hayatakuwa mazuri. 1.Naweza kufanya kila kitu mwenyewe. Hii inakuja pale mtu anapoanza kujiona yeye ni mzuri na mwelevu wa kila kazi katika biashara yake , lakini ukweli ni hauwezi kufanya kazi zote , ufagie , uhasibu,afisa utumisishi, afisa rasilimali watu na hata masoko wewe mwenyewe? Ukweli ni kwamba hauwezi ukawa mzuri wa hizo kazi zote ni lazima utakuwa na sehemu yako ambayo unaweza kufanya vizuri zaidi ya nyingine , na kama unataka biashara yako ifanikiwe fanya anbacho biashara inataka tumia au fanya ambacho unaweza kukifanya vizuri zaidi usilazimishe kwa kutaka kuonekana unajua sana au unaweza kufanya kuliko wengine ila fanya kwa kuangalia ni kipi unaweza kukifan...