Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara
Kuna mambo mengi ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina? Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio yote inayofanikiwa. Utakuta baada...