Vitu vinavyorudisha nyuma wajasiriamali/ wafanyabiashara (sehemu ya 2)
Toleo lililopita nilitoa maelezo kuhusu vitu ambavyo vinarudisha nyuma wajasiriamali wengi na wafanyabiashara, ambavyo ni vitu vya kawaida na vinafanyika na vingine hufanyika kimakosa bila hata kujua. Unapokuwa mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU atasaidia. Na madhara yote hutegemea vitu 4 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako Mipango biashara yako( Business plan) Baadhi ya vitu ambavyo huwa vinawafelisha wengi ni pamoja na jinsi ya utengenezaji au ufanyaji wake , japokuwa mpango biashara ndio nguzo ya biashara wengi hufikiria ni ufujaji wa p...