Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianz...