Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ujasiriamali na upungufu wa kazi kwa vijana.
Nchi yetu inaongozwa na sheria na moja kati ya sheria za nchi hii ni kila mtu ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake , hivyo na mimi nimeamua kutoa maoni yangu binafsi kuhusu hili suala la ujasiriamali hapa nchini , kwanza pongezi kwa serikali kuona njia mbadala ya kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ni kufanya ujasiriamali , lakini nilikaa na kuangalia baadhi ya mambo nikagundua kuna mapungufu mengi na mara nyingi tumezoea kutaja matatizo ili uliemwambia atafute suruhisho. Hapo unakuwa unakosea kama yeye hakuliona tatizo unapompa tatizo tu bila suruhisho unampa kazi ya kufanya ambacho hakijui hebu fikiria nimekutengenezea gari lako na kukuletea mimi sio mtengenezaji wa kwanza inamaanisha ntarekebisha ili liwe kama awali wewe ndio unaetumia gari yako nikitengeneza isipofika unapohitaji ni lazima utaniambia bado ilikuwa anafanya hivi na hivi na hivi tofauti kabisa na huku kuna tatizo la maji kijijini watu wanaeleza tu tunashida ya maji tufikiriwe hata kidogo na sisi tunatembea...