Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo
Marketing kwa maana moja mimi huwa naiita ni zao la Branding kwenye biashara ambalo linatakiwa litoke liende kuitangaza brand iliyojitengeneza.Hapa nchini biashara nyingi zinafanyika kwa mazoea na watu wanafanya bila kuelewa au kuwa na maana halisi ya kitu wanachokifanya, utakuta mtu ameona kampuni fulani wamefanya kitu fulani kwa ajili ya bidhaa, biashara au huduma kwa ajili ya kampuni yao, basi na yeye pia atataka kubadilisha jina tu kwenye hicho kitu kutoka jina la biashara alioiona hadi jina la biashara yake, ila vingine ataviaacha kama vya mwenzake kwa vile tu amependa jinsi kile kitu kilivyo. Na wengine hufanya hivyo kwa mifano na kujaribu . Leo nitaelezea kidogo vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kujitangaza au kufanya marketing,Tutaangalia vitu kama vitano(5) ambavyo unatakiwa kuviangalia kwenye biashara yako kabla ya kuanza kufanya marketing, vitu hivi mara zote huwa ni vitu vya kawaida na huonekana ni sio vya muhimu sana lakini nikupe siri ndugu yangu hakuna kitu a...