MABADILIKO YA MFUMO: TAHADHARI KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI
Habari za leo wana Branding, nimelazimika kurudia kupandisha uzi huu kutokana na hali ya mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi inavyoendelea hapa nchini, nimepokea maswali mengi kuhusiana na ishu ya mabadiliko yanayoendelea serikalini na kimfumo pia,majibu yangu hayakuwa mbali na tahadhari hii niliyoitoa mwezi Oktoba 2013 lakini leo imeleta majibu kwa kuanza kuonekana hebu pitia na uyasome tena kwa makini kwa maana bado mabadiliko yanaendelea kutokea.... tuwemo. Taa ya hatari imeanza kuwaka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Tanzania Asilimia kubwa ya wafanyabiashara, ( wakubwa na wadogo) wanafanya biashara Kienyeji na kikubahatisha wanafanya biashara kama mchezo wa bahati nasibu kupata Kukosa lakini siku sio nyingi mambo na hali itabadilika na kubadili mfumo wote wa kibiashara Hapa Tanzania. Kwa kuanza kwa sasa watanzaia wengi wanapata hamasa na hamu ya kuwa wafanyabiashara Au wajasiriamali kwa inspiration kutoka nchi za nje, kutoka kwa w...