Sehemu ya pili:Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko
Pia ningefurahi kupata mrejesho wako (feedback) juu ya uzi ninazotoa ili nijue pia kama jamii na mlengwa ninaemtegemea amepata elimu unaohitajika,kwa kuacha komenti yako hapo chini kwenye sehemu ya Comment, Asante. 8. Kueleza jina la kampuni yako Unapotengeneza nembo au unapotoa flyers na bidhaa nyingine inayokutambulisha kwenye soko hapo ni kuliweka jina la biashara au kampuni yako katika vichwa va wateja wako watarajiwa,ambapo ili mteja akutafute ni lazima awe anakukumbuka au anajina lako ndio anaweza kukutafuta mfano: Unaposikia bidhaa za Azam tayari unakumbuka na SSB Company ( Bakhresa). 9. Kutunza jina la kampuni yako kwa mteja Mteja mara zote anahitaji kitu cha kumkumbusha ili aweze kukukumbuka hivyo kwa kutoa vitu kama business card, flyer na vingine vya namna hiyo hapo unakuwa unatunza jina lako kwa mtu unaemtegemea na kwa yule uliempata na siri za kufanikiwa katika biashara ni kumfanya mteja akukumbuke kila anapofikiria huduma yako na huduma za pemb...