Kwanini usiache kuendelea kujitangaza na kutafuta masoko hata kama biashara yako inafanikiwa.
Nimekuwa nikiulizwa hili swali mara nyingi sana kuhusu mafanikio ya biashara na muendelezo wa matangazo, na asilimia kubwa ya wanaouliza swali hili ni wale ambao biashara zao zimefanikiwa au malengo waliyokuwa wameyaweka yamefikia au yamekaribia sana. Mara zote jibu langu huwa ni moja tu. Msingi wa biashara yako uko kwenye kujitangaza hivyo ukisimama kujitangaza basi na biashara itasimama kuingiza mauzo. Leo nimeona niweke hapa chini baadhi ya sababu ambazo zinakufanya kama mfanyabiashara au mjasiriamali usiache kuendelea kujitangaza. 1. Ushindani haukomi katika ulimwengu wa biashara mafanikio au kushindwa kunaletwa na ushindani,biashara isiyokuwa na ushindani haiwezi kujijua kama inashinda au inafeli sababu hakutakuwa na mwingine wa kuikumbusha kufanya ambavyo inatakiwa kufanya. Hivyo kama biashara yako iko sokoni na inafanya kazi kujitangaza hakukomi sababu mshindani wako kila siku anafikiria njia na namna ya kukushinda kibisahara mteja aliekuja kwako leo kesho awe ni mteja wake...