Posts

Showing posts from July, 2015

Hali za kimaisha za vijana zisitumike kama mtaji wa kisiasa kwa vyama na wanasiasa.

Image
Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa wewe ambae umeendelea kunitumia ujumbe mfupi ,kunipigia simu na kunitumia barua pepe kwa ajili ya shughuli hii,siwezi kuwataja wote kwa majina lakini ninautambua mchango wenu bila kusahau wapenzi wa blogu hii ambao huendelea kutembelea blogu hii hata kama sijaweka uzi upya niwashukuru kwa namna ya kipekee kabisa. Baada ya kupita kimya kidogo cha kutokuwa na uzi nimeonelea kwanza leo tuzungumze kidogo na vijana wa taifa hili maana hakuna familia isiyokuwa na kijana au vijana katika nchi hii, hata kama hatakuwepo kijana basi kutakuwa na kijana mtarajiwa.Tuko katika kipindi cha uchaguzi hivi sasa na watu wengi wanajitahidi kupata nafasi au sehemu ya kujishikiza kwa kipindi hichi ili angalau na wao wapate japo kidogo kitu katika mzunguko huu wa kampeni na mchakato wa uchaguzi kama mlivyoona kwa sasa kuna kampeni na zoezi la uandikishaji wapiga kura ambapo zinatumika mashine za BVR asilimia kubwa ya waandikishaji...