Posts

Showing posts from October, 2015

Vitu vinavyoenda sambamba katika brand

Kuna vitu vitatu ambayo hutumika sambamba   ili kutengeneza brand yenye afya 1.      Logo - Nembo Nembo   ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako 2.      Branding- kulijengea jina utambulisho Branding ni kutengeneza uaminifu na ahadi ya bidhaa yako kwenye akili ya mteja unaemtegemea Ambapo brand huunganishwa na bidhaa kwa mteja . 3.      Identity - utambulisho ( marketing,advertising,publication,sales) Hii inamaanisha aina ya utambulisho utakaotumia kujitambulisha, unaweza kujitambulisha kama expert Kujitambulisha kama mzoefu kujitambulisha kwa aina ambayo wewe itakupa ahueni na upenyo kwenye soko ulilopo. 4.      Kutokubadilika M oja ya vitu ambavyo vinatakiwa viangaliwe kwa umakini moja wapo ni kutokubadilika, brand inatengenezwa na utofauti wako katika eneo lako la ushind...

Kazi za branding

Brand   hutambulisha muonekano ,ubora   wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)   hazijulikani   na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa.  Ungana nami zaidi kupitia ukurasa wangu wa facebook : Elisha  Chuma ("like" ukurasa huu na utapata habari zote na machapisho  mara tuu ninapotoa.) Asante

Maana ya Branding katika Biashara/ujasiriamali wako

Image
Brand ni rasilimali inayotokana na ahadi ambayo inaunganishwa na bidhaa kwa wateja wake. Au brand ni alama inayotambulisha nafasi yako kwenye soko lako la ushindani. Shughuli ya brand inatakiwa iwe imedizainiwa na kuandaliwa maalum   kwa ajili ya biashara yako k ukutofautisha na wapinzani wako kibiashara. Hata kama wapinzani wote wanamuonekano Mzuri au kukushinda wewe . 1.   Brand yenye mafanikio huzingatia sanaumoja, Inapojitambulisha haijitambulishi  kwa vitu vingi Mfano :1.   Kampuni ya Cocacola wanabidhaa nyingi lakini ukiona  matangazo yao wamejikita sana kwenye  kuitangaza cocacola  yenyewe. ikiwa inamaanisha japo wanabidhaa nyingi bidhaa  zote zinajitengenezea au zinatengenezewa brand yake yenyewe. 2.      Kuna tofauti kati ya mauzo na kubrand. Rolex Orijino Rolex feki Mfano: unaweza kuuza saa ya Rolex dola 100? Ni kweli inawezekana kuuzwa kwa bei hiyo    na ...

Utangulizi elimu ya Branding

Habari za Jumatatu tena wana Branding, kwanza niwashukuru wote ambao mmekuwa mkinitafuta na kuulizia machapisho yangu mengine na kuomba semina mbalimbali inatia moyo zaidi kuona kama kazi ninayoifanya inaleta mafanikio katika soko kwa njia moja au nyingine, na baada ya kuwa kimya kwa kipindi kidogo sasa nitaendelea na kutoa machapisho na baada ya kuangalia kwa kipindi kirefu kuhusiana na Biashara na ujasiriamali bila kugusia kabisa elimu ya Branding ambayo ndiyo mzizi na kiini cha blogu hii. Kuanzia leo nitaanza mfululiza ma machapisho kuhusiana na elimu ya Branding kwa watu wote ambapo sasa ndipo tutapata kiini cha mafanikio na uendeshaji wa biashara kwa kila mfanyabiashara awe mjasiriamali au awe mjasiriamali, nitakuwa nikiweka machapisho hapa na pia kwa email kwa wale ambao watakuwa wamejisajili katika email pia kwa Facebook kwa wale walio like page yangu ( Elisha chuma) . Asanteni sana na kaeni mkao wa kula