Posts

Showing posts from 2016

Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 5)

5. Tengeneza brand ya promosheni Katika kazi zako zote usitake zote zitoke kwa pamoja ni lazima uchague moja ambayo itakutambulisha na ndio utakayoifanyia promosheni na matangazo sana,mara nyingi na imeshazoelekwa kwa nchi za kwetu huku kampuni moja kuwa na biashara zaidi ya moja yaani kuwa na vibali ama kutumia jina moja kufanya biashara ama kutoa huduma kwa kada zaidi ya moja, Mfano utakuta kampuni ni Nyarubamba Company na inahusika na Ushauri wa kifedha,usaili, na huduma za kibenki,hapo sasa kampuni ni moja lakini inafanya kazi 3 kwa wakati mmoja,sasa basi katika ulimwengu wa biashara kila tawi la hizo biashara ni biashara kamili hivyo ushauri wa kifedha ni biashara kamili, Usaili ni biashara kamili na pia huduma za kifedha ni biashara kamili kwa muonekano ni kama vile zote ziko kwenye mlengo mmoja wa fedha lakini zinatofautiana utendaji wake wa kazi, sasa basi unachotakiwa kufanya ni lazima uchague tawi moja ambalo utakuwa unalifanyia promosheni na sio yote, yaani u...

Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 4)

4. Tengeneza vipengele 3 vya  brand vilivyobaki. Baada kuziangalia zile  hatua 3 hapo nyuma ukishazipitia zote sasa unaingia katika kutengeneza vipengele  3 vya brand vilivyosalia ambavyo ni Brand ya mtu, Brand ya bidhaa na brand ya mfumo.ili kuikamilisha Brand nzima kwa ufasaha ni lazima uwe umejitosheleza katika vipengele vyote vya Branding. sasa basi Brand ya mtu inawakilisha muonekano wako na jinsi unavyowahudumia wateja ambapo kila kitu unachokifanya unatakiwa utambue kinapokelewa kama ujumbe katika masikio na maisha ya watu,hivyo ni lazima wewe  mwenyewe ujibrand kufikisha ujumbe sawasawa na ahadi ya brand yako, kama brand inasema usafi na wewe ni lazima uwe msafi na kama brand inasema huduma bora ni lazima huduma bora ionekane kwako bidhaa haileti hivyo vyote,japo bidhaa ndio inakuwa na muonekano wa kumvutia lakini haiwezi kumuongelesha hivyo mteja akipenda lazima atawasiliana na wewe hapo ndipo brand ya mtu inapopata nafasi zaidi. Brand y...

IPENDE BIASHARA YAKO

Image
Hakuna kitu kizuri kama kuitangaza biashara yako kitaalamu na kwa mvuto zaidi, biashara zote zinalipa ila inategemeana na unaipenda biashara yako kiasi gani, tujenge mazoea ya kurudisha kwa ajili ya biashara mfano, unapotangaza viatu,mafuta ama nguo hata kama sio vya kwako ila ukitengeneza na nembo yako ukawa kila unachopost kinakuwa nayo hautengenezi muonekano tu bali unatengeneza na hadhi pia, asilimia kubwa ya biashara tuzifanye kwa ajili ya vizazi vijavyo pia bila kuwa na msingi hata wa muonekano biashara inamaanisha ukichoka na yenyewe inachoka lakini kukiwa na msingi hata wa page rasmi ya bidhaa ni rahisi kuendelezwa,pia inapoteza uzito unapotangaza unauza kitu mathalani cha laki 1,2 hadi milioni ila umekipiga picha tu na simu yako hata hakionekani vizuri,tengeneza muonekano wa biashara yako leo ili ujisaidie mwenyewe na vizazi vijavyo. Tengeneza nembo yako vizuri iwe na muonekano thabiti ili ikidhi vigezo za kada yako,dizaini mtindo ambao utautumia kujitangaza ama ...

Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 3)

3. Chagua sehemu sahihi ya kujibrand Kila biashara inasehemu yake ambayo inajitosheleza hata biashara yako pia inasehemu ambayo ukiiweka inatosha kabisa hivyo chagua kwa makini sehemu ambayo unaiweka biashara yako ili usije kupishana na biashara yako. Ili kujua sehemu sahihi ya kuiweka biashara yako no lazima utambue vitu vifuatavyo ili kukupa mwanga wa unakoelekea. 1. Aina ya wateja wako 2. Hali zao kiuchumi 3. Wanapatikana wapi 4. Unawapataje 5. Nnatumia mbinu gani? Ukishayajibu maswali hayo kwa ufasaha utatambua eneo lako ambalo ni sahihi kujitangaza japo kwa hali ya sasa teknolojia ndio sehemu ambayo wateja wengi wanapatikana hata huko pia kuna matabaka, wateja walioko Facebook ni tofauti na wateja walioko Linkeldin na tofauti na wateja walioko Instagram hivyo usikurupuke kwa kufuata biashara ya mwenzako kwamba kwa vile alifanya kupitia kile akafanikiwa na mimi basi nitafanikiwa hapana utafeli sababu kila biashara ina njia zake za kutokea. leo nitaishia hapa toleo lij...

Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 2)

2. Anza kujirasmisha  Kabla ya kuingia sokoni ni vizuri sana ukiwa umejirasmisha nikiwa namaanisha ukiwa umejiweka rasmi kwa kuingia katika ushindani maana biashara ni ushindani usiposhinda basi utakuwa hauna nafasi katika biashara hiyo ambapo kwako ambae ndio mgeni ama mchanga katika hilo usipojirasmisha mapema inamaanisha unaenda kufeli pale utakapokutana na washindani wako ambao tayari wapo kwa muda mrefu na wamejirasmisha ukiingia kichwa kichwa utajikuta unatumia gharama kubwa kupata nafasi katika soko ambapo ilikuwa ni rahisi kwa kujirasmisha na kutumia upenyo wa soko ambao umeiweka biashara yako. Nnaposema kujirasmisha nnamaanisha ni kutengeneza vitu ambavyo vitakuweka rasmi katika soko, vitakupa uhalali wa kuwa sokoni na baadhi ni vitu ambavyo mteja atahitaji avione mwanzoni pale anapokutana na biashara yako ambavyo kwa ushauri wangu  ni pamoja na 1. Logo ( Nembo) 2. Businesscard 3. Identification( Vitambulisho) 4.  Letterhead( kichwa cha barua...

hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 1)

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza swali la napotaka kuanza kufanya Branding natakiwa nifanye kitu gani?, kitu cha kwanza ambacho ni msaada mkubwa kwako kwanza unatakiwa uijue Branding yenyewe ni nini, ndipo unaweza kutambua unatakiwa kuanzia wapi kisha ukaelekea wapi, lakini kwa kupunguza muda na kusaidia kuokoa wakati unaweza kufanya hivi. 1. Tengeneza brand plan Kitu cha kwanza ambacho unaweza kufanya unatakiwa uwe na mpango wa kila kitu unachokifanya usifanye kwa kukurupuka kwa vile watu wengine huwa wanafanya hapana utakuwa unakosea unatakiwa utengeneze mpango wa jinsi ya kujibrand,ili ukuongoze kwa hatua kulingana na soko lako pia malengo na maono ya biashara yako. ukiwa na brand plan itakusaidia kupata mwanga wa nini cha kufanya,wapi na kwanini. Brand plan inakusaidia wewe mwenyewe kuona mwanga wa biashara yako inaenda wapi inaongozwa na nini na ina sehemu gani katika soko, hivyo unapoitengeneza tayari unapata mwanga wa kutosha wa biashara yako pia inakusaidia kutengeneza baj...

Jinsi ya kujitangaza na ujumbe kumfikia mteja unaemtaka

Biashara nyingi zimekuwa zinafeli kufikia malengo ama kufanikiwa kwa sababu ya kutokutambua ni nani na aina gani ya ujumbe/ wateja ambao  ujumbe unatakiwa uwafikie. Kwa mjasiriamali kutambua uwanja wako wa kujitangaza ni jambo la muhimu sana, kama hujui utakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze ujumbe utatoka lakini hautawafikia walengwa hivyo utakuwa hauna matokeo chanya yoyote sababu waliouona hauwahusu, sababu kutambua uwanja wako ndicho kitu cha kwanza ambacho hukupa muelekeo na maandalizi safi ya kampeni na promosheni zako. Kwanini ni muhimu biashara kutambua aina ya uwanja na watu inaowataka? ili kufanya tangazo lako liwe na mashiko ni lazima lionekane kwa mtu sahihi, na ukishatambua ndipo hapo unaweza kutengeneza ujumbe na muonekano utakaoendana na malengo ya uwanja wako. Ili kujua aina na mteja wako unaetakiwa kumfikishia ujumbe ni lazima utambue na kuzifuata hatua zifuatazo. 1. Chagua aina( Kifaa cha mawasiliano) Unatakiwa kuwalisiliana na watu na hii itakuwa...

Je tangazo lako katika mitandao ya kijamii linawafikia walengwa

Watu wengi sasa hivi wanatumia mtandao wa facebook kujitangaza na kutafutia wateja, Karne ya 21 imeonyesha ukuaji wa teknolojia katika kila nyanja elimu,mawasiliano,usafiri nakadhalika.kutokana na hilo biashara nyingi zinatafuta na kujitengenezea brand na wateja kupitia hapa lakini kila kitu kina changamoto zake unapojitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuna vitu ambavyo unatakiwa ufuatilie ili kupata matokeo chanya ya tangazo au biashara yako. 1. Aina ya wateja wako kulingan a na asili na kiwango cha biashara yako. 2. Hadhi ya wateja wako 3.Uwanja wa matarajio yako 4. Muundo wa kazi zako 5. Muda sahihi wa kutoa au kujitangaza 6. Muitikio wako. Ukivizingatia hivyo hapo juu basi mitandao ya kijamii itakupa matokeo chanya siku zote, punguza gharama za kutengeneza kampeni za masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Jinsi ya kujitangaza na wapi pa kujitangaza

Utafutaji wa masoko umebadilija sana kipindi cha hivi karibuni kutoka mauzo mengi kwa ushawishi wa mdomo hadi kwenye kujitangaza kupitia mtandao. Asilimia kubwa ya wateja sasa hivi wanapatikana kwenye mtandao na asilimia kubwa ya biashara zinajitangaza kwenye mitandao,hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na upatikanaji wa taarifa nyingi muhimu kwa urahisi. Njia nyingine inayotumika ni kujitangaza kupitia mteja wako,biashara nyingi sasa hivi ziko kwenye utaratibu wa kutoa kamisheni kwa mteja atakae leta mteja mwingine,kwa sababu marketing ya mteja huwa ya uhakika na ya uzoefu hivyo humvuta mtu zaidi kutumia bidhaa au huduma. Hivyo ukiangalia njia zote mbili hapo juu ni kama zinaua soko la watu wa masoko badala yake linaongeza soko kwa watu wa teknolojia na habari hali imebadilika hii inakuja pia kama changamoto kwa sekta nyingine ya waliomo ndani ya kada ya kutafuta masoko na wanaofikiria kujiunga yafaa kuangalia zaidi mbele na dunia itahitaji nini zaidi kutoka kwako kwa muda gani...

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake. Hali ya mzunguko na mfumo wa biashara imebadilika sana hapa nchini na hii imechangiwa na kuongezeka kwa makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakiongeza chachu ya kuendelea kufanya zaidi ya pale wazawa wanapofanya, na tofauti kubwa ambayo inafanya kampuni nyingi na biashara nyingi za nje kufanikiwa ni Branding, asilimia kubwa ya hizo kampuni huingia nchini tayari zikiwa zimeshajibrand hivyo inakuwa rahisi kupata nafasi katika soko la ndani. Kinyume cha hapo asilimia kubwa ya biashara au kampuni zetu wazawa hazijafanya Branding ambayo ndio uti wa mgongo wa biashara, matokeo yake imekuwa hatuwezi kuuza ndani sababu hazina muonekano mzuri na hatuwezi kuuza nje sababu pia hazijafanyiwa branding nzuri. Baada ya serikali kuiona changamoto hiyo ikaanza kusisitiza wafanyabiashara kufanya branding vizuri( kuboresha  utengenezaji na upakiaji wa bidhaa uwe mzuri na wa kuvutia ili bidhaa zetu zipate nafasi hata katika soko la nje kwa wingi). Hivyo ...

Nembo yako inamaanisha nini?

Je wewe ni mfanya biashara au mjasiriamali au mfanyabiashara?umetengenezaje nembo yako? inakidhdi vigezo vya soko lako? Kwanza Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi. Kwanini biashara yako inahitaji nembo 1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako 2.Huonyesha muonekano unaotakiwa 3.hukuongezea hadhi 4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko 5.Kuwa na muonekano wa kuvutia 6.Hujipanga yenyewe kwa malengo flani ya soko. Vitu vya kuangalia unapotengeneza logo 1. Iwe ya kipekee 2. Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma 3. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea 4. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati) 5. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja y...

Mafanikio ya biashara yako na muonekano wake

Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana muonekano wako ambao hutengeneza uaminifu,heshima na kumvuta mteja, iwapo muonekano ukiwa tofauti na lengo mteja husita kufanya hivyo vilivyopo hapo juu, kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinachukuliwa cha kawaida katika kuipandisha na kuipa muonekano biashara yako ni fani ya Graphics design. fani hii kwa sasa imekuwa ni kama imeingiliwa kila anaetumia kompyuta basi anaweza kuwa graphics designer,hili limepelekea hadi sasa ubora wa muonekano na uhalisia wa kwanza wa biashara unapotea. Nguzo kuu ya Graphics design ni lazima dizaina awe anajua Branding,Maumbo,Mpangilio,fonts na rangi lakini sasa hivi vingi vinapuuzwa na kulifanya soko kuwa la kawaida,Je katika vitambulishi  vyako vyote viko sawa kulingana na maana ya rangi,maumbo,mpangilio na fonts kufuatana na uasili wa biashara yako? Makampuni makubwa husimamia zaidi suala la muonekano wao wanapokupa kazi wanatoa hadi na vipimo muonekano unaotakiwa na vipimo vya rangi ili usibadilishe mu...

Je unafahamu biashara yako inatakiwa iwe na muoneako gani ili iuze?

Serikali ya awamu ya 5 inapeleka mambo kasi na inathamisha katka mifumo tuliyoizoea na kutupeleka katika mifumo mipya, moja kati ya mabadiliko yanayoongelewa sana na yanayohitajika sana ni kukuza pato la taifa na kupandisha thamani ya pesa yetu hii inamaanisha ni kupunguza uagizaji na kuongeza uzalishaji kutokana na hilo serikali inashauri biashara ziongeze kujitangaza na kuuza nje ya mipaka ya Tanzania ili tuongeze kupokea malipo ya Usd kuliko sisi kulipa Usd.  Sasa basi moja kati ya kada zinazoangaliwa katika hili ni kada ya biashara ambapo inapokea urasmishaji na uboreshwaji wa mipango ya kimaendeleo kwa kasi sana hivyo biashara nyingi ambazo hazikuwa zimejipanga sawasawa kwenda na kasi yoyote nyingi zitakufa, lakini katika urasimishaji huu biashara haiongelei sana bidhaa ila inaongelea vitambulishi vya bidhaa, Katika mkutano wa wafanyabiashara kutoka India uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana rai yao ilikuwa ni kuboresha upakiaji na vifungashio vya bidhaa zetu hivyo kinachole ta...

Itambue kanuni kuu ya pesa

Kila kitu katika dunia hii kina kanuni aidha unaijua au hauijui, unaitambua au hauitambui leo nitaiongelea kanuni kubwa kabisa ya kwanza ya pesa. Kwanza kabisa nikubadilishe mawazo kuhusu upatikanaji na dhana ya mzunguko wa pesa. Kwanza ukubaliane na mimi kwanza kuhusu pesa kwamba, pesa uliyonayo mkononi,mfukoni,benki ama sehemu yoyote ile ambayo unaweza kuitoa kama unavyojiita mmiliki ile pesa sio ya kwako sababu kila pesa unayoishika tayari inasehemu au kazi ya kufanya na kama inasehemu au kazi ya kufanya inamaanisha inabidi ile pesa itoke mkononi mwako, hivyo wewe ni muwakilishi tu umeishika kwa muda huo ili uipeleke kwa mwingine, mfano Ukipewa 10,000 sasa hivi unajihisi kama wewe ni mmiliki wake lakini katika ulimwengu wa fedha wewe umekuwa daraja la mzunguko wake, hivyo kama ni daraja inabidi uipitishe ambapo lazima utaitoa na kumpa mtu mwingine hiyo pesa ambae hata yeye akiisha kuishika inakuwa sio yake tena inabidi akaitoe mfano umeenda kununua unga ukampa 10,000 atakurudishi...

Jinsi ya kutengeneza matokeo chanya kupitia business card yako.

Je unaitumiaje fursa ya kujitangaza kupitia Business card yako.japo bzcard ni kikaratasi kidogo kinaweza kukupa matokeo chanya zaidi ya vingine kwanza ni kidogo NA pia ni rahisi kukitunza tofauti na vingine hivyo ukikipa muonekano na maelezo sahihi kina matokeo chanya zaidi.lakini tuangalie hapa chini kwann tunakosea. kwanza Wengi wetu tumefanya business card kama karatasi ya namba tu,Ndio.Kwa nchi zilizoendelea bzcard imebeba namba tu labda na website.lakini kwa huku kwetu hali iko tofauti watu wengi hawakokaribu sana na matumizi ya mtandao zaidi wanatumia mtandao kupitia mitandao ya kijamii,hii inapunguza fursa ya kuitembelea tovuti yako. Pili asilimia kubwa ya watengenezaji na watengenezewaji huhisi bzcard ni bzcard tu haijalishi,lakini iko tofauti hata dizaini za bzcard zinatofautiana kulingana na kada tofauti tofauti,ukikosea kuitengeneza usitegemee kama atakaeiona atakufikiria kupitia kada yako.Mfano biashara ya chakula ikatengeneza bzcard kama za benki utaigusa ile bzcard unap...

Jifunze kufanikiwa kwa kiwango ulichopo

Kila biashara hutegemea kufanikiwa katika eneo lake la ushindani lakini asilimia kubwa hufeli kwa vile hazitambui mafanikio yanahitaji vitu gani,chache ambazo hutambua uhitaji wa mafanikio hufanya ushindani na kujitengenezea nafasi katika soko, leo nitatoa siri 7 za vitu ambavyo vitakutengenezea mafanikio kwa sehemu na kiwango ulicho nacho kwa sasa:- 1.IBRAND BIASHARA YAKO. Branding sio neno geni na nimeshalitaja na kulielezea sana hivyo itengenezee muonekano wa tofauti katika soko lako, utofauti wako kwenye soko utakao kupa nafasi katika soko lako la ushindani na mafanikio ni matokeo ya ushindani. 2.UTAFITI Usifanye vitu kwa mihemko au kukurupuka  fanya utafiti wa kutosha kuhusu biashara yako  kuanzia vitu kama Eneo,Asili ya biashara, wateja wako,ushindani na aina zote za washindani, Mbinu shirikishi na vingine vingi, mafanikio hayawezi kuja iwapo hautajua uko katika kiwango gani na unakutana na ushindani aina gani,hilo unaweza kulielewa kwa kufanya utafiti tu hivyo t...

Jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia

Habari tena wanabranding, natumai mu wazima bukheri wa afya leo nimeona tukumbushane kidogo baadhi ya vitu ambavyo vitatusaidia wote kwa pamoja kuongeza masoko na kukuza uchumi wa taifa hili. Mada yetu leo inasema jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia siku baada ya siku. Utandawazi umebadilisha mambo mengi sana katika maisha ya mwanadamu na miongoni mwa vitu ambavyo viliguswa ni pamoja na sekta ya biashara ambapo kadri mambo na siku zinavyoenda nayo inaenda inabadilika hasa kwa huku kwetu nchi zinazoendelea. Teknolojia imekuja kurahisisha baadhi ya kazi na utendaji kazi wa eneo fulani miaka ya nyuma ilikuwa kama unahitaji kusajili kampuni yako ni lazima uende Brela ukaandike jina, utume barua, wakujibu ndio uanze kuomba usajili lakini sasa hivi kila kitu unakifanyia nyumbani kwa kutumia kompyuta yako tu. Tra nao vivyo hivyo ilikuwa ni lazima uende ofisi zao ili kulipa kodi lakini sasa unaweza kutuma hata kwa simu, hayo ni baadhi ya mabadiliko ya teknoloj...

Je! unajua maana ya Meme/Motto/Slogan katika biashara yako?

Watu wengi wamekuwa wanafanya vitu bila kutambua maana na kwanini, leo nitatoa dondoo kidogo kuhusu meme/Slogan/Motto. Hiki sio kitu kigeni lakini wengi tumwekuwa tukikifanyia mazoea leo pata darasa kidogo. Kila biashara inapofanyiwa branding lengo kuu liko kwa mteja na unapotaka kumpata mteja yoyote lazima uchanganye ahadi,ubora na picha. Ahadi hutolewa na Slogan au meme ya biashara, hivyo meme yako inamaana kubwa sana katika kuisimamisha biashara yako mfano. Katika magari Ukiwa unaendesha Marcedez Benz hata kama ni ya mwak 1921 bado slogan yake ni "expensive car" hata kama kiuhalisia sio kweli ila kwa vile brand yao ilitoa meme ya hivyo mteja anaweza kwenda kununua sio kwa sababu anaipenda Marcedez hapana ila tu ni kwa sababu its expensive car, gari aina ya BMW ni "comfortable car" nayo pia vivyo hivyo. Sasa basi nafikiri umepata picha ni kiasi gani meme inaweza kuathiri picha ya biashara yako aidha ukiifanya vibaya au vizuri. Chini hapa nakuwekea muongoz...

Maelezo kuhusu darasa la ujasiriamali.

Kama nilivyowaarifu hapo awali kutakuwa na darasa la branding na ujasiriamali kwa  watu wote wanaotegemea kuwa wafanyabiashara au wajasiriamali... nitatumia mtandao wa whatsapp kuendesha darasa hilo na litakuwa la mwezi mmoja kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupitia whatsapp Gharama za darasa itakuwa ni 25,000 kwa wiki 1 hivyo  kwa mwezi 1 ni sawa na 100,000 unaruhisiwa kulipia kila wiki . Faida za darasa hili ni 1.utajitambua mwenyewe uko kundi gani kati ya mjasiriamali au mfanyabiashara. 2.Utakuwa na uwezo wa kuona fursa na kupata wazo sahihi. 3.Kutambua aina za washindani katika biashara yako, na wapi ni hatari zaidi. 4.Pia utapokea sababu nyingi zinazofelisha wafanyabiashara wengi. 5.utapata muongozo wa kuanzisha na kusimamia biashara yako. 6.utapata ushauri binafsi 7.utapata muda wa kuuliza maswali yanayokutatiza. 8.Utapata muongozo wa Branding katika biashara. 9.Utapata nafasi ya kufahamiana na kubadilishana changamoto na wajasiriamali wengine. 10.Kila ...

Taarifa kwa Wasomaji wa blogu hii

Habari njema kwa wote mliokuwa mkifuatilia makala na matoleo yangu kuhusu ujasiriamali kupitia,blogu,kundi la whatsapp na  facebook.baada ya kuwa kimya kwa muda kidogo sasa nitaendelea tena kutoa makala na machapisho kupitia blogu yetu ya  www.elishachuma.blogspot.com  kuanzia mwezi wa pili  , na pia natarajia kuanzisha darasa la branding na ujasiriamali kwa wafanyakazi na wale wanaotegemea kuwa wafanyabiashara au wajasiriamali... nitatumia mtandao wa whatsapp kuendesha darasa hilo na litakuwa la mwezi mmoja kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupitia whatsapp number 0713603699. Branding ni kubwa sana kwa muonekano na kufikirika lakini ukiijua vizuri unaweza kubrand biashara yako katika hatua yoyote na ukafanikiwa,Karibu.