Jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia
Habari tena wanabranding, natumai mu wazima bukheri wa afya leo nimeona tukumbushane kidogo baadhi ya vitu ambavyo vitatusaidia wote kwa pamoja kuongeza masoko na kukuza uchumi wa taifa hili. Mada yetu leo inasema jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia siku baada ya siku. Utandawazi umebadilisha mambo mengi sana katika maisha ya mwanadamu na miongoni mwa vitu ambavyo viliguswa ni pamoja na sekta ya biashara ambapo kadri mambo na siku zinavyoenda nayo inaenda inabadilika hasa kwa huku kwetu nchi zinazoendelea. Teknolojia imekuja kurahisisha baadhi ya kazi na utendaji kazi wa eneo fulani miaka ya nyuma ilikuwa kama unahitaji kusajili kampuni yako ni lazima uende Brela ukaandike jina, utume barua, wakujibu ndio uanze kuomba usajili lakini sasa hivi kila kitu unakifanyia nyumbani kwa kutumia kompyuta yako tu. Tra nao vivyo hivyo ilikuwa ni lazima uende ofisi zao ili kulipa kodi lakini sasa unaweza kutuma hata kwa simu, hayo ni baadhi ya mabadiliko ya teknoloj...