Jifunze kufanikiwa kwa kiwango ulichopo
Kila biashara hutegemea kufanikiwa katika eneo lake la ushindani lakini asilimia kubwa hufeli kwa vile hazitambui mafanikio yanahitaji vitu gani,chache ambazo hutambua uhitaji wa mafanikio hufanya ushindani na kujitengenezea nafasi katika soko, leo nitatoa siri 7 za vitu ambavyo vitakutengenezea mafanikio kwa sehemu na kiwango ulicho nacho kwa sasa:- 1.IBRAND BIASHARA YAKO. Branding sio neno geni na nimeshalitaja na kulielezea sana hivyo itengenezee muonekano wa tofauti katika soko lako, utofauti wako kwenye soko utakao kupa nafasi katika soko lako la ushindani na mafanikio ni matokeo ya ushindani. 2.UTAFITI Usifanye vitu kwa mihemko au kukurupuka fanya utafiti wa kutosha kuhusu biashara yako kuanzia vitu kama Eneo,Asili ya biashara, wateja wako,ushindani na aina zote za washindani, Mbinu shirikishi na vingine vingi, mafanikio hayawezi kuja iwapo hautajua uko katika kiwango gani na unakutana na ushindani aina gani,hilo unaweza kulielewa kwa kufanya utafiti tu hivyo t...