Mafanikio ya biashara yako na muonekano wake
Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana muonekano wako ambao hutengeneza uaminifu,heshima na kumvuta mteja, iwapo muonekano ukiwa tofauti na lengo mteja husita kufanya hivyo vilivyopo hapo juu, kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinachukuliwa cha kawaida katika kuipandisha na kuipa muonekano biashara yako ni fani ya Graphics design. fani hii kwa sasa imekuwa ni kama imeingiliwa kila anaetumia kompyuta basi anaweza kuwa graphics designer,hili limepelekea hadi sasa ubora wa muonekano na uhalisia wa kwanza wa biashara unapotea. Nguzo kuu ya Graphics design ni lazima dizaina awe anajua Branding,Maumbo,Mpangilio,fonts na rangi lakini sasa hivi vingi vinapuuzwa na kulifanya soko kuwa la kawaida,Je katika vitambulishi vyako vyote viko sawa kulingana na maana ya rangi,maumbo,mpangilio na fonts kufuatana na uasili wa biashara yako? Makampuni makubwa husimamia zaidi suala la muonekano wao wanapokupa kazi wanatoa hadi na vipimo muonekano unaotakiwa na vipimo vya rangi ili usibadilishe mu...