Jinsi ya kujitangaza na wapi pa kujitangaza
Utafutaji wa masoko umebadilija sana kipindi cha hivi karibuni kutoka mauzo mengi kwa ushawishi wa mdomo hadi kwenye kujitangaza kupitia mtandao. Asilimia kubwa ya wateja sasa hivi wanapatikana kwenye mtandao na asilimia kubwa ya biashara zinajitangaza kwenye mitandao,hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na upatikanaji wa taarifa nyingi muhimu kwa urahisi. Njia nyingine inayotumika ni kujitangaza kupitia mteja wako,biashara nyingi sasa hivi ziko kwenye utaratibu wa kutoa kamisheni kwa mteja atakae leta mteja mwingine,kwa sababu marketing ya mteja huwa ya uhakika na ya uzoefu hivyo humvuta mtu zaidi kutumia bidhaa au huduma. Hivyo ukiangalia njia zote mbili hapo juu ni kama zinaua soko la watu wa masoko badala yake linaongeza soko kwa watu wa teknolojia na habari hali imebadilika hii inakuja pia kama changamoto kwa sekta nyingine ya waliomo ndani ya kada ya kutafuta masoko na wanaofikiria kujiunga yafaa kuangalia zaidi mbele na dunia itahitaji nini zaidi kutoka kwako kwa muda gani...