Je tangazo lako katika mitandao ya kijamii linawafikia walengwa
Watu wengi sasa hivi wanatumia mtandao wa facebook kujitangaza na kutafutia wateja, Karne ya 21 imeonyesha ukuaji wa teknolojia katika kila nyanja elimu,mawasiliano,usafiri nakadhalika.kutokana na hilo biashara nyingi zinatafuta na kujitengenezea brand na wateja kupitia hapa lakini kila kitu kina changamoto zake unapojitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuna vitu ambavyo unatakiwa ufuatilie ili kupata matokeo chanya ya tangazo au biashara yako. 1. Aina ya wateja wako kulingan a na asili na kiwango cha biashara yako. 2. Hadhi ya wateja wako 3.Uwanja wa matarajio yako 4. Muundo wa kazi zako 5. Muda sahihi wa kutoa au kujitangaza 6. Muitikio wako. Ukivizingatia hivyo hapo juu basi mitandao ya kijamii itakupa matokeo chanya siku zote, punguza gharama za kutengeneza kampeni za masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.