Posts

Showing posts from August, 2016

Jinsi ya kujitangaza na ujumbe kumfikia mteja unaemtaka

Biashara nyingi zimekuwa zinafeli kufikia malengo ama kufanikiwa kwa sababu ya kutokutambua ni nani na aina gani ya ujumbe/ wateja ambao  ujumbe unatakiwa uwafikie. Kwa mjasiriamali kutambua uwanja wako wa kujitangaza ni jambo la muhimu sana, kama hujui utakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze ujumbe utatoka lakini hautawafikia walengwa hivyo utakuwa hauna matokeo chanya yoyote sababu waliouona hauwahusu, sababu kutambua uwanja wako ndicho kitu cha kwanza ambacho hukupa muelekeo na maandalizi safi ya kampeni na promosheni zako. Kwanini ni muhimu biashara kutambua aina ya uwanja na watu inaowataka? ili kufanya tangazo lako liwe na mashiko ni lazima lionekane kwa mtu sahihi, na ukishatambua ndipo hapo unaweza kutengeneza ujumbe na muonekano utakaoendana na malengo ya uwanja wako. Ili kujua aina na mteja wako unaetakiwa kumfikishia ujumbe ni lazima utambue na kuzifuata hatua zifuatazo. 1. Chagua aina( Kifaa cha mawasiliano) Unatakiwa kuwalisiliana na watu na hii itakuwa...