IPENDE BIASHARA YAKO
Hakuna kitu kizuri kama kuitangaza biashara yako kitaalamu na kwa mvuto zaidi, biashara zote zinalipa ila inategemeana na unaipenda biashara yako kiasi gani, tujenge mazoea ya kurudisha kwa ajili ya biashara mfano, unapotangaza viatu,mafuta ama nguo hata kama sio vya kwako ila ukitengeneza na nembo yako ukawa kila unachopost kinakuwa nayo hautengenezi muonekano tu bali unatengeneza na hadhi pia, asilimia kubwa ya biashara tuzifanye kwa ajili ya vizazi vijavyo pia bila kuwa na msingi hata wa muonekano biashara inamaanisha ukichoka na yenyewe inachoka lakini kukiwa na msingi hata wa page rasmi ya bidhaa ni rahisi kuendelezwa,pia inapoteza uzito unapotangaza unauza kitu mathalani cha laki 1,2 hadi milioni ila umekipiga picha tu na simu yako hata hakionekani vizuri,tengeneza muonekano wa biashara yako leo ili ujisaidie mwenyewe na vizazi vijavyo. Tengeneza nembo yako vizuri iwe na muonekano thabiti ili ikidhi vigezo za kada yako,dizaini mtindo ambao utautumia kujitangaza ama ...