Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 5)
5. Tengeneza brand ya promosheni Katika kazi zako zote usitake zote zitoke kwa pamoja ni lazima uchague moja ambayo itakutambulisha na ndio utakayoifanyia promosheni na matangazo sana,mara nyingi na imeshazoelekwa kwa nchi za kwetu huku kampuni moja kuwa na biashara zaidi ya moja yaani kuwa na vibali ama kutumia jina moja kufanya biashara ama kutoa huduma kwa kada zaidi ya moja, Mfano utakuta kampuni ni Nyarubamba Company na inahusika na Ushauri wa kifedha,usaili, na huduma za kibenki,hapo sasa kampuni ni moja lakini inafanya kazi 3 kwa wakati mmoja,sasa basi katika ulimwengu wa biashara kila tawi la hizo biashara ni biashara kamili hivyo ushauri wa kifedha ni biashara kamili, Usaili ni biashara kamili na pia huduma za kifedha ni biashara kamili kwa muonekano ni kama vile zote ziko kwenye mlengo mmoja wa fedha lakini zinatofautiana utendaji wake wa kazi, sasa basi unachotakiwa kufanya ni lazima uchague tawi moja ambalo utakuwa unalifanyia promosheni na sio yote, yaani u...