Wazo la biashara 01
Asilimia 80% ya dawa tunazotumia mahospitalini zinatokana na miti,na asilimia 60 ya magonjwa tunayougua yanatokana na mtindo wa maisha, hivyo ukiwa kama mjasiriamali ama mfanyabiashara unatakiwa uone fursa hapo katikati ya kuugua na miti. Matunda yanatumika sana kama dawa, na chakula ni dawa ndio maana ukikikosea kinakuwa sumu mwilini sasa tupitie fursa hii,ikakufungue na kukupa maono mapya. FURSA: Unaweza kuuza ujuzi ama kuwa mshauri wa masuala ya chakula,matunda na miti. JINSI YA KUIFANYA: Kama mtumiaji wa mtandao anza kwa kutafuta na soma kwa makini matumizi,faida,utengenezwaji,uhifadhi na mfumo wa mwanadamu unavyopokea na unatumia nini kwa matunda ambayo yanapatikana sana eneo lako ama yanayopatikana kwa urahisi ( Mfano kuchanganya tunda lenye ukali na lisilokuwa na ukali unaliua lile tunda lisilokuwa na ukali linakuwa pombe(Nanasi na ndizi).),fuatilia na chakula uandaaji,viungo,upishi na kadha wa kadha hakikisha unatambua kila aina ya chakula tunda ...