Posts

Showing posts from February, 2017

Wazo la 3

Vijana wengi na watu wengi wamekuwa na shida ya ajira sasa hivi ambapo imefikia hatua inabidi aajiriwe katika sekta isiyokuwa na weledi wake na wengine kukosa kabisa,wengine wanapesa za mitaji lakini hawana wazo bora la biashara waanzishe kitu gani ili kiwe na mafanikio kwao. Leo hii tutaenda kuangalia wazo jingine la biashara ambalo litawahusu sana akina mama na akina dada,katika mzunguko wa maisha wote tunatakiwa kutambua Mungu ni kiongozi na katika uumbaji wake hakuna alieumbwa kwa bahati mbaya na ndani ya kila mtu kuna kitu cha ziada ambacho Mungu amemuwekea kulingana na utashi wake..Leo nitawapa mbinu ya kujiajiri kwa madada ambao wanasema hawana ajira kabisa. Kuna baadhi ya kazi ambazo kama mdada ama mwanamke ukifanya kwa uhakika zinakutoa na hazihitaji chuo wala cheti ni kipaji na baraka tu baadhi ya kazi hizo ni pamoja na ususi,kutengeneza vitafunwa(bites),kufanya usafi na kadhalika,kama wewe unajijua unakitu unachoweza kukifanya kwa ufasaha kwa moyo wote bila kushurti...