ENEO LA BIASHARA
Kumekuwa na changamoto kubwa kuhusiana na lipi ni eneo sahihi la kuiweka biashara yako,watu wamekuwa na kasumba na kujifanyia hadi imefikia hatua hawajui athari zimeletwa na nini. Na hii inachangiwa mara nyingi na kufanya vitu bila kufuata weledi ama kuonana na washauri wa masuala hayo,mara nyingi biashara zinapoanza mwenye biashara hutafuta kuwa na sehemu tu ya kumfanya aonekane na yeye ana sehemu ya uelekezi (Physical address) lakini inapokuja suala la kwanini amechukua eneo hilo huwa hana majibu ya moja kwa moja kama inamfaa ama haimfai kwa kulingana na biashara yake. Hili limekuwa tatizo kubwa sana na madhara yake yanaweza kuwa hayako moja kwa moja ila yanakutafuna mfano: ukiwa kwenye location sio unaweza kuwa unapata wateja wa mwisho na wa kwanza wanaishia kwa mwenzako,hii itasababisha biashara kuwa na mauzo ya kawaida na kutokukua ,ikichelewa kukua inamaanisha malengo yatapishana na mipango ambapo kufeli kwake kunakuwa mlangoni lakini chanzo cha yote ni ku...