Posts

Showing posts from 2019

Aina ya malengo ya kujiwekea unapomaliza mwaka

Image
 Wengi wetu inapofika mwisho wa mwaka hufikiria kuanza upya na kurekebisha sehemu tulizokosea ili mwaka unaofuata uwe wa mafanikio zaidi ya ule unaoishia ama kupita lakini malengo yetu huwa yanajichanganya sababu ya kukosa muongozo thabiti wa kuyafikisha mahala pake na mengi huishia kuwa matarajio ambapo matarajio yasipo kutana na malengo yanakuwa mawazo,wengi tunaangukia kwenye mawazo sababu hatupangi leo nakupa malengo ambayo unapomaliza mwaka hakikisha umeyaandika ili kukukuza wewe,biashara,kazi,imani na kadha wa kadha. hakikisha umezingatia maeneo makuu 7 tofauti ya kujiwekea malengo na kuhakikisha kila eneo unaweka mikakati thabiti itakayokuwezesha kufikia hayo malengo yako. Maeneo muhimu ya kujiwekea malengo ni: 1. Malengo ya Kiroho (Spiritual Goals) 2. Malengo ya Familia/Ndoa (Family/Marriage Goals) 3. Malengo ya Fedha (Financial Goals) 4. Malengo ya Maendeleo Binafsi (Personal Development Goals) 5. Malengo ya Kimwili/Kiafya (Physical/Health Goals) 6. Malengo ya Kazi...

Hekima ya baba huonekana kwa mtoto

Image
HEKIMA YA BABA HUONEKANA KWA MTOTO Ukiwa mzazi mara nyingi hupenda kutumia ukali,fimbo na nyenzo kadha wa kadha katika kuwaelewesha watoto wetu Katika makuzi yao. Lakini leo nakupa changamoto kama mzazi kile kinachoonekana kwa mwanao ndio kile ulichokihitaji. Nadhana zinasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini mimi ninaenda ndani zaidi ili kujenga zaidi,Hekima ya baba huonekana kwa mtoto,hivyo usipomfundisha hekima yako usitegemee yeye kujifunza kwa dunia. Wengi tumekulia malezi ya fimbo na ukali kiukweli zinasaidia lakini hazijengi Sana,fimbo zinatengeneza uoga,hofu,kutokujiamini,amri lakini hata uwezo mdogo wa kufikiri,haya na madhara ambayo huonekana baadae Sana hekima ya baba inakua ni uoga,hofu,kutojiamini na kadhalika ambapo vijana wa Leo ndio tatizo kubwa ufahamu ( mentality) zimeharibika tangu wakiwa wadogo,halafu wakifika ukubwani gafla wanatakiwa wajitegemee ni mtihani mkubwa zaidi kwao sababu hekima ya baba imepungua sana, tunakimbilia sana kuwalaumu watoto bila kutafuta c...

Maisha huongeza thamani unapopita kwenye bonde la uvuli wa mauti.

Image
Mara nyingi mwanadamu akichomwa na mwiba ndio huona thamani ya kandambili (ndala) lakini kabla ya hapo zinaitwa malapa ya kuendea chooni. Hali hii imeendelea kwa vitu vingi tunavyovohisi muda mwingine ni vidogo na havina thamani lakini tunavihitaji sana,asilimia kubwa yetu uhai na pumzi tunayovuta tunaichukulia kawaida,kulala na kuamka salama tunaona kawaida kwa vile ni kitu kinachojirudia kila siku na wengine hata wanapopata matatizo hukimbilia hata kuwaza kwanini wanaishi ama maisha kwao hayana thamani,wanasindikiza wanaoishi na maneno kadha wa kadha,lakini siku unayopewa sababu ya kuona maisha yako yanakatishwa na kitu kifulani aidha ugonjwa,ajali,maradhi n.k ndio uthamani wake huja. Iko vivyo hivyo kwenye kila kitu unachokifanya kipe uthamani kabla hakijapotea elimu yako ni ya thamani sana usisubiri hadi ufe ndio tuone madaftari ya mipango yako mizuri,Anza kufanyia kazi ukiwa hai,Afya yako ni ya thamani usisubiri hadi uwe hospitali ndio uanze kuuona uthamani wake,Anza kuitunza afya...

Elisha Chuma: Simamia wazo kuu

Wengi huwa tunakimbia wazo mama na kukimbilia mawazo mtambuka bila kukumbuka bila wazo mama mtambuka lisingeonekana. Simamia wazo kuu,unapelitenda wazo mtambuka hakikisha wazo kuu haliathiriwi. Elisha Chuma +255 745108010

Tofauti ya Ukweli na uhalisia

Ishi kiuhalisia endana na uhalisia wako,huenda ukweli unakuvuta ili usimame mahala ama kuonyesha uwezo lakini uhalisia ndio sehemu pekee unayoweza kuwa na amani na kutengeneza mafanikio yako. Watu wengi wamefeli kwa kuusimamia ukweli kuliko uhalisia mathalani,ukweli ni kwamba unahitaji kula ili uishi uhalisia ni kwamba unahitaji kufanya kazi ili upate hela ya kukuwezesha kununua chakula ili uishi. Wasanii,wafanyabiashara na watu wengi wamefelishwa sana na hiki kitu na bado kinawatafuna wengi kuung'ang'ania ukweli ilhali uhalisia unakataa ndio matokeo yake unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako mwisho wa kuishi hivyo ni kufeli. Ishi maisha yako ya uhalisia utapata amani ya moyo na ni rahisi kutengeneza mafanikio na mbinu zake ukiwa kwenye uhalisia kuliko kwenye ukweli wako. #Maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe

Elisha Chuma : Kujiamini

Image
Je wewe unajiamini,unatambua faida  za kujiamini na hasara za kutokujiamini hebu pitia somo hili ujione uko sehemu gani. Kujiamini naweza kusema ni uwezo wa kuwa na uthubutu juu ya mambo pasipo kuwa na hofu wala uoga bila kutegemea msukumo kutoka nje. Kujiamini sio kitu cha kufanyiwa na mtu mwingine ila ni maamuzi binafsi ambayo yana hatua zake ukitaka kuyafikia ili ufikie hatua ya kujiamini vitu vinavyochangia ama vinavyoweka chachu na hamasa ya wewe kujiamini ni pamoja na     1. Kujitambua    2. Maamuzi binafsi    3. Imani yako    4. Uelewa    5. Makuzi na   6. Mazingira  Hivyo ndio vitu ambavyo unapofikiria kujiamini vinakupa chachu na hamasa wewe kufanya jambo bila msukumo wa nje bali msukumo wa ndani yako mwenyewe. Vitu vinavyoweza kukusaidia kujiamini katika maisha yako. 1. Jifunze kujithamini ( usijione huna thamani hata siku moja) 2. Jisamehe na kuwa mkweli kwa nafsi yako mweny...

Kwanini 40 ?

Image
Kwanini vitu vinaangukia siku ya 40 Muda na wakati unatupa mkono sana katika kuijua kweli na hii inasababishwa na vitu vingi mabadiliko ya uchumi,hali ya hewa,mitindo ya maisha,kuiga na vichocheo vingi vinatufanya tunabadilisha ile kweli kuwa kawaida, leo nitaongelea suala la kwanini mtoto anapozaliwa anatakiwa kuwekwa ndani kwa siku 40 ni kitu ambacho tumekikuta tumekirithi lakini tunakiacha, Je vizazi vyetu ama kizazi chako cha 4 kitafahamu kama kulikuwa na kuweka 40 kama kuanzia kwako haujaweka 40?. Historia,zama na ukweli vinatupeleka mbali sana lakini hii dhana ya 40 haijatumika kwa mtoto tu vipo vingi leo tutaangalia kwanini 40. Sasa basi katika   ulimwengu war oho kuna kitu kinaitwa Aura hiki kiko kwenye mwili wa hauwezi kukishika wala kukigusa ni kama tabaka lililopo juu ya mwili wako ambalo linakusaidia na kukukinga na nguvu za nje,mfano unaweza kutembea ukahisi mwili umesisimka ghafla tambua hapo aura yako imefanya kazi,ama umepima na unaumwa lakini hujany...

Namna bora ya kujitangaza

Image
Soko limebadilika sana kulinganisha na zamani watu wengi sasa hivi wameanza kutambua umuhimu wa kjitangaza na biashara nyingi sasa zinafanya branding(Chapa), kwa ajili ya kupata nafasi katika soko husika, lakini tunashida moja, hatujaweza kuwatumia washauri wa mambo ya biashara ipasavyo, tunapungua sana. Watu wengi wamekuwa na shida kuhusiana na jinsi ama namna bora ya kujitangaza sababu ya kutokutambua ni lini utangazaze, saa ngapi ? na nani anaetakiwa kuona na sio hivyo tu bali hata kwa njia gani.  Hali hii inachangiwa kwa namna moja ama nyingine na  mfumo wa biashara lakini pia kuna visababishi kama soko la utangazaji kukosa watu wengi wenye weledi wa jinsi ya kujitangaza lakini wateja kuwa na maamuzi zaidi ya kile ambacho soko linahitaji pia  matumizi ya wataalam na watoa ushauri kwa habari ya biashara na branding. Biashara nyingi zimejikuta zinafeli si kwasababu hazina bidhaa nzuri hapana ni kwa sababu hazijitangazi vizuri, sasa...

Aina za malengo na mipango

Image
Aina za Malengo na mipango Katika maisha ya kila siku kila mtu hutengeneza malengo na mipango ya kufikia kilele fulani,lakini kutokana na kutokuwa na aina kamili ama sahihi za malengo na mipango watu wengi hujikuta malengo na mipango yao inafeli kwa sababu hujiandaa kwa vitu vichache kuliko uhalisia wenyewe. asilimia kubwa ya watu hutengeneza mipango bila malengo na matokeo yake ile mipango hufeli sababu hakuna malengo kamili,katika maisha ya kila siku kuna mipango ya aina 2 (mbili) na katika malengo kuna malengo ya aina 7 (saba). hivyo unapofikiria kutengeneza mipango na malengo yako ili ukue na kufikia kile unachokihitaji ni lazima malengo yote yakamilike ndio mipango itafanikiwa kwa ufasaha. Aina za Mipango - hizi sio aina ngeni kabisa kwa watu japo wengi hawajui kuzitumia na kuitofautisha,kuna mipango aina 2,mipango ya muda mrefu na mipango ya muda mfupi,ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa ndio imebeba lengo kuu kwa vile safari ya ku...

Jifunze kupokea matatizo kama changamoto

Image
Jifunze kuwa mjasiriamali mzuri,ukiyabadilisha mazingira na unayoyaita matatizo kuwa changamoto,utaanza kuziona fursa kupitia changamoto yako,badilisha aina ya mawazo yako usiishi ndani ya boksi la uwezo na uelewa wako toka nje ya boksi lako utaona vitu katika hali ya tofauti sana. Mfano mdogo ni masikini siku zote anaomba majaribu ama matatizo yasimpate ili aendelee kusimamia eneo lake,lakini anaefanikiwa anatamani changamoto za kiwango cha juu ili atatue na kupanda kiwango,hali hii inakuja hata kwenye nyumba za ibada wanaojihisi hawana wanawaachia michango wanaohisi wanacho mwisho wa siku aliekuwa nacho anaongezewa na asiekuwa anacho ananyang'anywa. kila kinachopita kwako ni thawabu inategemea na vile unavyokichukulia aidha kitakujenga ama kitakubomoa,chagua kujengwa ili kesho uwe bora zaidi ya jana,hakuna asiekuwa na changamoto ila tofauti ni jinsi ya kuzipokea na kuzifanyia kazi. Elisha Chuma Snr www.elishachuma.blogspot.com

Elisha Chuma : Maana ya mawasiliano

Image
Watu wengi wanapowasiliana mawazo yao ama fikra zao huwapeleka kwenye kujibu kabla ya kuelewa kwanza na ndipo hujitokeza ile dhana uanongea na mtu unahisi anakuelewa halafu baada ya muda ndio anakufata anakwambia "kwa hiyo kumbe pale ulimaanish hivi" hii ni dalili moja wapo kwamba  mtu huyu hakukusikiliza ili akuelewe ila akujibu kwanza,mimi na wewe ni mashahidi wa vitendo hivi mara nyingi na kulingana na mazingira tumejikuta tumesahau kurekebisha tabia hii ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa watu wengi. Kwenye usaili sasa hivi kampuni nyingi zinatumia mbinu ya kupima uwezo wa mtu kuelewa kama kigezo moja wapo cha kumuajiri  mtu,maswali utakayoulizwa asilimia kubwa ni ya kukupima kiwango chako cha uelewa hii yote ili kuhakikisha ni mtu sahihi nje ya weledi alionao,unaweza kuwa na ujuzi ama uwezo mkubwa wa kufanya kazi ila kama hautakuwa mtu wa kuwasiliana kwa kuelewa inamaanisha ile dhana ya "team work" inakuwa inapotea sababu hautaweza kufanya kazi vizuri na...

Tofauti kati ya ukweli na uhalisia

Ishi kiuhalisia endana na uhalisia wako,huenda ukweli unakuvuta ili usimame mahala ama kuonyesha uwezo lakini uhalisia ndio sehemu pekee unayoweza kuwa na amani na kutengeneza mafanikio yako. Watu wengi wamefeli kwa kuusimamia ukweli kuliko uhalisia mathalani,ukweli ni kwamba unahitaji kula ili uishi uhalisia ni kwamba unahitaji kufanya kazi ili upate hela ya kukuwezesha kununua chakula ili uishi. Wasanii,wafanyabiashara na watu wengi wamefelishwa sana na hiki kitu na bado kinawatafuna wengi kuung'ang'ania ukweli ilhali uhalisia unakataa ndio matokeo yake unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako mwisho wa kuishi hivyo ni kufeli. Ishi maish a yako ya uhalisia utapata amani ya moyo na ni rahisi kutengeneza mafanikio na mbinu zake ukiwa kwenye uhalisia kuliko kwenye ukweli wako. #Maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe

Muonekano wako ndio biashara yako

Image
Biashara nyingi zimefeli sokoni sababu ya kutengeneza muonekano hafifu ama unaokinzana na aina ya asili ya biashara husika na bahati mbaya matokeo ya makosa ya branding huwa hayaonekani moja kwa moja kama ilivyo branding (chapa) yenyewe, chapa inatengenezwa ndani ya kichwa cha mtu hivyo kufeli na kufaulu kwake ni ndani kwa ndani ndio maana mara nyingi hufanywa kwa kufuata saikolojia ya mawazo ya mtu. Sasa basi imekuwa ni ndoto ya watu wengi sana kuwa ama kuanzisha biashara zao,lakini na wengine tayari wameshaanzisha baadhi ya vitu ambavyo hutiliwa maanani sana kwa wengi ni upande wa bidhaa/huduma pamoja na eneo la huduma kwa sababu wazo la biashara haliji na muonekano hivyo huweka juhudi kwenye vitu ambavyo huhisi ama kuona ni vya muhimu sana,lakini sehemu ambayo huchukuliwa kawaida ni sehemu ya muonekano bila kujua biashara inalindwa na kusimamiwa na muonekano kwanza ndio vingine vinafuata,unapokosea kutengeneza muonekano ama chapa yako vizuri unakuwa kwenye hatihati ya kupoteza n...