Elisha Chuma : Maana ya mawasiliano
Watu wengi wanapowasiliana mawazo yao ama fikra zao huwapeleka kwenye kujibu kabla ya kuelewa kwanza na ndipo hujitokeza ile dhana uanongea na mtu unahisi anakuelewa halafu baada ya muda ndio anakufata anakwambia "kwa hiyo kumbe pale ulimaanish hivi" hii ni dalili moja wapo kwamba mtu huyu hakukusikiliza ili akuelewe ila akujibu kwanza,mimi na wewe ni mashahidi wa vitendo hivi mara nyingi na kulingana na mazingira tumejikuta tumesahau kurekebisha tabia hii ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa watu wengi. Kwenye usaili sasa hivi kampuni nyingi zinatumia mbinu ya kupima uwezo wa mtu kuelewa kama kigezo moja wapo cha kumuajiri mtu,maswali utakayoulizwa asilimia kubwa ni ya kukupima kiwango chako cha uelewa hii yote ili kuhakikisha ni mtu sahihi nje ya weledi alionao,unaweza kuwa na ujuzi ama uwezo mkubwa wa kufanya kazi ila kama hautakuwa mtu wa kuwasiliana kwa kuelewa inamaanisha ile dhana ya "team work" inakuwa inapotea sababu hautaweza kufanya kazi vizuri na...