Aina za malengo na mipango
Aina za Malengo na mipango Katika maisha ya kila siku kila mtu hutengeneza malengo na mipango ya kufikia kilele fulani,lakini kutokana na kutokuwa na aina kamili ama sahihi za malengo na mipango watu wengi hujikuta malengo na mipango yao inafeli kwa sababu hujiandaa kwa vitu vichache kuliko uhalisia wenyewe. asilimia kubwa ya watu hutengeneza mipango bila malengo na matokeo yake ile mipango hufeli sababu hakuna malengo kamili,katika maisha ya kila siku kuna mipango ya aina 2 (mbili) na katika malengo kuna malengo ya aina 7 (saba). hivyo unapofikiria kutengeneza mipango na malengo yako ili ukue na kufikia kile unachokihitaji ni lazima malengo yote yakamilike ndio mipango itafanikiwa kwa ufasaha. Aina za Mipango - hizi sio aina ngeni kabisa kwa watu japo wengi hawajui kuzitumia na kuitofautisha,kuna mipango aina 2,mipango ya muda mrefu na mipango ya muda mfupi,ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa ndio imebeba lengo kuu kwa vile safari ya ku...