Aina ya malengo ya kujiwekea unapomaliza mwaka
Wengi wetu inapofika mwisho wa mwaka hufikiria kuanza upya na kurekebisha sehemu tulizokosea ili mwaka unaofuata uwe wa mafanikio zaidi ya ule unaoishia ama kupita lakini malengo yetu huwa yanajichanganya sababu ya kukosa muongozo thabiti wa kuyafikisha mahala pake na mengi huishia kuwa matarajio ambapo matarajio yasipo kutana na malengo yanakuwa mawazo,wengi tunaangukia kwenye mawazo sababu hatupangi leo nakupa malengo ambayo unapomaliza mwaka hakikisha umeyaandika ili kukukuza wewe,biashara,kazi,imani na kadha wa kadha. hakikisha umezingatia maeneo makuu 7 tofauti ya kujiwekea malengo na kuhakikisha kila eneo unaweka mikakati thabiti itakayokuwezesha kufikia hayo malengo yako. Maeneo muhimu ya kujiwekea malengo ni: 1. Malengo ya Kiroho (Spiritual Goals) 2. Malengo ya Familia/Ndoa (Family/Marriage Goals) 3. Malengo ya Fedha (Financial Goals) 4. Malengo ya Maendeleo Binafsi (Personal Development Goals) 5. Malengo ya Kimwili/Kiafya (Physical/Health Goals) 6. Malengo ya Kazi...