Posts

Showing posts from 2020

Jiandae kufeli

Image
Biashara,Mahusiano,Mipango mingi inafeli sababu watu hawajiandai na changamoto za anachokitafuta ama kukifanya matokeo yake anawaza faida tu,zinapokuja changamoto zake anajikuta anafeli kirahisi sana Biashara nyingi zinapoandaliwa huwa ni kw mpango wa "high season" mauzo yako juu lakini uhalisia hakuna biashara ambayo inakuwa kwenye high season mwaka mzima ni lazima kuwe na kipindi cha "low season" mauzo hafifu na hapo ndio biashara nyingi hufa,kwa kuwa hazikujiandaa na low season matokeo yake ni kula mtaji na kupumzika,hili ni janga la biashara nyingi...UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WAZA NA KIPINDI CHA KUFELI AMA KUPOROMOKA KWA BIASHARA UTAFANYA NINI?. Kwenye mahusiano wapenzi wengi huingia wakitegemea raha tu na furaha na mara nyingi mwanzo wa mahusiano kila mtu hujitahidi kufanya ili kumridhisha mwenzake,ila baada ya muda ile hali ya kuridhishana huisha huingia hali ya uhalisia hapo ndio shida huanza,vikwazo,wivu,husda,vijitabia huonekana,sasa kwa kuwa akili ya weng...

Mafanikio na gharama zake.

Image
Nimekuwa nikikutana na kujadiliana na watu wengi sana kuhusu mbinu na jinsi ya kufanikiwa,nimegundua watu wengi wanayapenda sana mafanikio na wanatamani kufanikiwa lakini hawakotayari kuzibeba gharama za mafanikio hayo. Kufinikiwa ni kupiga hatua na hakuna hatua inayopigwa bila kutumia nguvu,hata hatua ya mguu wako ili unyanyuke unahitaji nguvu,balance,uelekeo na mambo kadha iko hivyo pia kwenye mafanikio. Ili ufanikiwe lazima uzikubali gharama za eneo lako la mafanikio,usiwe kwenye kundi la kutamani kila siku na ku"wish" jitoe kwenye hiyo hali kwa kubadilisha mawazo yako. Na ili ufanikiwe utakavyo tumia gharama kutengeneza mafanikio yako,usiombe kila kitu wakati wewe unatengenezewa kitu. Mafanikio yanaanza na mabadiliko ya tabia na mtazamo,anza kufanikiwa ndani yako sasa ili uyatengeneze mafanikio ya nje. Elisha Chuma. Mwalimu,Mshauri & Kocha wa Mafanikio 

Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme

Image
Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme. Watu wengi kwenye mahusiano huchanganya kipi kinahitajika wapi na kipi kinawekwa wapi,ugomvi na kutokuelewana vinachukua sana nafasi sababu kila mtu hajui anakosea wapi na anajiona yuko sahihi. Iko hivi utambue leo. Mwanaume maisha yake yote hahitaji kupendwa,uhitaji wake mkubwa kwenye mahusiano sio kuonyeshwa anapendwa ama kufanyiwa vitu vya kudhihirisha upendo wako,atavichukulia kawaida wakati wewe umevichukulia pakubwa sana na utalalamika hupendwi,kumbe umemkosea hitaji la mwanaume kwenye mahusiano ni "Heshima" mwanaume anahitaji kuheshimiwa tu,ukimuheshimu kwake ni tafsiri ya unampenda ndio maana ili kumlegeza mwanamme na kukupa unachotaka mwanamke akishusha sauti na akaongea kwa upole,ustaarabu na utii mwanaume hufanya kile mwanamke anachokitaka sababu ameonyesha heshima,hivyo mwanamke usipambane kuonyesha unampenda ila onyesha unamheshimu. Lakini hali iko tofauti pia kwa mwanamke yeye anapenda kwa hisia na kudhahania,...

Hatua za kufuata unapofikiria kuanza kufanya biashara yoyote

Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara, tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye biashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu. Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kinaugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka,hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni,hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako. Wazo la biashara. Kitu cha kwanza unachotakiwa utafute ni wazo la biashara,hii itategemea na eneo pamoja na asili ya kazi yako (kwa muongozo wa jinsi ya k...