Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme
Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme. Watu wengi kwenye mahusiano huchanganya kipi kinahitajika wapi na kipi kinawekwa wapi,ugomvi na kutokuelewana vinachukua sana nafasi sababu kila mtu hajui anakosea wapi na anajiona yuko sahihi. Iko hivi utambue leo. Mwanaume maisha yake yote hahitaji kupendwa,uhitaji wake mkubwa kwenye mahusiano sio kuonyeshwa anapendwa ama kufanyiwa vitu vya kudhihirisha upendo wako,atavichukulia kawaida wakati wewe umevichukulia pakubwa sana na utalalamika hupendwi,kumbe umemkosea hitaji la mwanaume kwenye mahusiano ni "Heshima" mwanaume anahitaji kuheshimiwa tu,ukimuheshimu kwake ni tafsiri ya unampenda ndio maana ili kumlegeza mwanamme na kukupa unachotaka mwanamke akishusha sauti na akaongea kwa upole,ustaarabu na utii mwanaume hufanya kile mwanamke anachokitaka sababu ameonyesha heshima,hivyo mwanamke usipambane kuonyesha unampenda ila onyesha unamheshimu. Lakini hali iko tofauti pia kwa mwanamke yeye anapenda kwa hisia na kudhahania,...