Jiandae kufeli
Biashara,Mahusiano,Mipango mingi inafeli sababu watu hawajiandai na changamoto za anachokitafuta ama kukifanya matokeo yake anawaza faida tu,zinapokuja changamoto zake anajikuta anafeli kirahisi sana Biashara nyingi zinapoandaliwa huwa ni kw mpango wa "high season" mauzo yako juu lakini uhalisia hakuna biashara ambayo inakuwa kwenye high season mwaka mzima ni lazima kuwe na kipindi cha "low season" mauzo hafifu na hapo ndio biashara nyingi hufa,kwa kuwa hazikujiandaa na low season matokeo yake ni kula mtaji na kupumzika,hili ni janga la biashara nyingi...UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WAZA NA KIPINDI CHA KUFELI AMA KUPOROMOKA KWA BIASHARA UTAFANYA NINI?. Kwenye mahusiano wapenzi wengi huingia wakitegemea raha tu na furaha na mara nyingi mwanzo wa mahusiano kila mtu hujitahidi kufanya ili kumridhisha mwenzake,ila baada ya muda ile hali ya kuridhishana huisha huingia hali ya uhalisia hapo ndio shida huanza,vikwazo,wivu,husda,vijitabia huonekana,sasa kwa kuwa akili ya weng...