Posts

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe  ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu  anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu  yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianz...

Nukuu za Chuma

Image

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa.

Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kutambua pesa kama mtaji wa kila kitu katika biashara , lakini katika ulimwengu wa biashara iko tofauti pesa sio mtaji bali pesa ni kiasidizi cha mtaji . Leo nitakupa baadhi ya njia unazoweza kutumia kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa ila kwa kutumia mtaji mbinu na vinginevyo. Watu wengi  huruka sana sehemu ya kwanza ya mtaji ambayo ndio  chimbuko la mtaji  na kukimbilia kwenye  sehemu zinazofuata na kuendelea bila kujua muhimili wa nyumba ni msingi bila ya msingi mzuri nyumba inaanguka hivyo bila chimbuko zuri la mtaji wako hauwezi kufanikiwa, sasa basi chimbuko hilo ni nini ambalo watu huliruka na kukimbilia mengine. Kichwa/ akili mtaji wako mkubwa ni kichwa chako na hata wazo na kila kitu kinaratibiwa na kichwa chako mwenyewe ndani ya kichwa ndipo panatengeneza ndoto na ndipo panapofanya ndoto zitimie kwa kushirikiana na viungo vingine vya mwili lakini injini ya mwanadamu ni kichwa katika kufanya mambo ya ...

Vitu vinavyorudisha nyuma wajasiriamali/ wafanyabiashara (sehemu ya 2)

Toleo lililopita nilitoa maelezo kuhusu vitu ambavyo vinarudisha nyuma wajasiriamali wengi na wafanyabiashara, ambavyo ni vitu vya kawaida na vinafanyika na vingine hufanyika kimakosa bila hata kujua. Unapokuwa mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU atasaidia. Na madhara yote hutegemea  vitu 4 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako Mipango biashara yako( Business plan) Baadhi ya vitu ambavyo huwa vinawafelisha wengi ni pamoja na jinsi ya  utengenezaji au ufanyaji wake , japokuwa mpango biashara ndio nguzo ya biashara wengi hufikiria ni ufujaji wa p...

Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara

Kuna mambo mengi ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana   wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina? Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio yote inayofanikiwa. Utakuta baada...

Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako

Iwe ya kipekee Watu wengi wamezoea kuwa wanatengeneza logo kwa kuigilizia ya sehemu fulani au kwa kufuatisha mfumo wa kampuni fulani , wengine hufanya kama logo nyingine kisa tu ni kwa vile imempendezea machoni kwake au ameipenda bila kujali ujumbe utakaotoka baada ya hapo, nembo yako mara zote inatakiwa  iwe ya kipekee na isifanane na nembo yoyote dunia nzima. Hasa katika soko ulilopo, unatakiwa kuifuata maana halisi ya nembo kama nembo ni utambulisho wako iweje uwe unafanana na utambulisho wa mwingine na iwapo umeigilizia kutoka kwa mwenzako inamaanisha tayari yeye brand yake ni kubwa kuliko yako hivyo ukitengeneza nembo inayofanana nayakwake ni kama vile unamsaidia kumkumbushia watu na kumtengenezea nafasi katika vichwa vya wateja wake. Mfano: leo hii ukipita sehemu ukaona nembo inayofanana na ile nembo ya brand ya cocacola utamkumbuka nini brand ya cocacola au brand ya yule aliyeitengeneza . Ukweli ni kwamba utaikumbuka cocacola na unaweza hata kuanza kujiuliza kam...

Muendelezo wa umuhimu wa Logo katika biashara yako

Image
Kukutambulisha katika soko Logo yako ndio inayokutambulisha katika soko la ushindani ,soko la biashara  na hata kwa wateja hivyo logo yako inatakiwa iwe ambayo ni maalum kweli ili utambulisho wako usije kuwa na muonekano mbaya au usiovutia logo yako ndio ambayo inatathminiwa ndani ya soko mtu anapoiona logo yako ndio anakutambua. Logo ni muongozi wa biashara yako  kwa sababu unapokutana na mteja ananunua kitu kutokana na utambulisho na muendelezo wa logo ya bidhaa unayotengeneza siku sio nyingi nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiemfahamu akawa anataka nimtengenezee logo kawaida yangu huwa ni kupata maelezo nikamuuliza ameipatia wapi namba yangu na aina ya logo anayotaka alishangaa kidogo kuona nakuwa na maswali kumzidi lakini alielewa na kitu alichokuja kunijibu ni aliona business card yangu kwa mtu akawa amependa logo yangu ikawa imemvutia kiasi kwamba akawa anataka nayeye  nimtengenezee nyingine lakini iwe jamii ya hiyo ya kwangu, hivyo logo yako ni ...