Posts

Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ujasiriamali na upungufu wa kazi kwa vijana.

Nchi yetu inaongozwa na sheria na moja kati ya sheria za nchi hii ni kila mtu ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake , hivyo na mimi nimeamua kutoa maoni yangu binafsi kuhusu hili suala la ujasiriamali hapa nchini , kwanza pongezi  kwa serikali kuona njia mbadala ya kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ni kufanya ujasiriamali , lakini nilikaa na kuangalia baadhi ya mambo nikagundua kuna mapungufu mengi na mara nyingi tumezoea kutaja matatizo ili uliemwambia atafute suruhisho. Hapo unakuwa unakosea kama yeye hakuliona tatizo unapompa tatizo tu bila suruhisho unampa kazi ya kufanya ambacho hakijui hebu fikiria nimekutengenezea gari lako na kukuletea mimi sio mtengenezaji wa kwanza inamaanisha ntarekebisha ili liwe kama awali wewe ndio unaetumia gari yako nikitengeneza isipofika unapohitaji ni lazima utaniambia bado ilikuwa anafanya hivi na hivi na hivi tofauti kabisa na huku kuna tatizo la maji kijijini watu wanaeleza tu tunashida ya maji tufikiriwe hata kidogo na sisi tunatembea...

Kwanini wajasiriamali wengi wanafeli?

Image
Kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa  wanahitaji kuwa wajasiriamali lakini asilimia kubwa wanakuwa ni wale ambao wanakuwa wamefeli mipango mikubwa au kuna kitu kimewasukuma ,vitu ambavyo unatakiwa usifanye kwa kudhani unatengeneza maisha utakuwa unapotea. Kuna kundi ambalo wao huanza ujasiriamali baada ya kuona umri unaenda au wanategemewa sasa na aidha famili a au kadahali Usifanye ujasiriamali kwa kuona umri umeenda upate kitu cha kujishikiza, hapo utafeli kumekuwa na watu wengi ambao hadi astaafu ndio anaanza ujasiriamali au baada ya kuona umri umeenda ndio anatafuta kitu cha kumpatia ujasiriamali hii ni mbaya na kufanikiwa kwake ni kugumu sana, ujasiriamali sio nyongeza ya ulichonacho ujasiriramali ni msingi wa ulichonacho kama hukutengeneza msingi mwanzo ujue hata uweke ukuta imara kiasi gani dhoruba ikija ni lazima nyumba itapata mtikisiko. Wapo wengine ambao wanafanya ujasiriamali  baada ya kukosa au kutuma sana maombi ya kazi ukifany...

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe  ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu  anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu  yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianz...

Nukuu za Chuma

Image

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa.

Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kutambua pesa kama mtaji wa kila kitu katika biashara , lakini katika ulimwengu wa biashara iko tofauti pesa sio mtaji bali pesa ni kiasidizi cha mtaji . Leo nitakupa baadhi ya njia unazoweza kutumia kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa ila kwa kutumia mtaji mbinu na vinginevyo. Watu wengi  huruka sana sehemu ya kwanza ya mtaji ambayo ndio  chimbuko la mtaji  na kukimbilia kwenye  sehemu zinazofuata na kuendelea bila kujua muhimili wa nyumba ni msingi bila ya msingi mzuri nyumba inaanguka hivyo bila chimbuko zuri la mtaji wako hauwezi kufanikiwa, sasa basi chimbuko hilo ni nini ambalo watu huliruka na kukimbilia mengine. Kichwa/ akili mtaji wako mkubwa ni kichwa chako na hata wazo na kila kitu kinaratibiwa na kichwa chako mwenyewe ndani ya kichwa ndipo panatengeneza ndoto na ndipo panapofanya ndoto zitimie kwa kushirikiana na viungo vingine vya mwili lakini injini ya mwanadamu ni kichwa katika kufanya mambo ya ...

Vitu vinavyorudisha nyuma wajasiriamali/ wafanyabiashara (sehemu ya 2)

Toleo lililopita nilitoa maelezo kuhusu vitu ambavyo vinarudisha nyuma wajasiriamali wengi na wafanyabiashara, ambavyo ni vitu vya kawaida na vinafanyika na vingine hufanyika kimakosa bila hata kujua. Unapokuwa mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU atasaidia. Na madhara yote hutegemea  vitu 4 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako Mipango biashara yako( Business plan) Baadhi ya vitu ambavyo huwa vinawafelisha wengi ni pamoja na jinsi ya  utengenezaji au ufanyaji wake , japokuwa mpango biashara ndio nguzo ya biashara wengi hufikiria ni ufujaji wa p...

Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara

Kuna mambo mengi ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana   wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina? Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio yote inayofanikiwa. Utakuta baada...