Posts

Salamu na mambo ya kuzingatia mwaka 2015

Kwanza kabisa sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwepo kwa mwaka huu hadi kuiona krismas nyingine tena ya mwaka huu, wapo wengi waliotamani kuiona lakini hawajaifikia. Ila zote ni baraka za Mwenyezi Mungu. Tukirudi katika mada kuu nawatakieni heri ya Krismasi na Mwaka mpya wa 2015 wasomaji wangu wapendwa,wajasiriamali,wafanyabiashara na kila anaepitia na kusoma hapa, nawatakia sherehe njema na nnawaombea tufike wote mwaka 2015. Nimekuwa kimya kidogo nilikuwa na shughuli zimenibana kidogo lakini nafikiri kwa baadhi waliokuwa wanapata shida kunipata walikuwa wanatumia mawasiliano yangu ambayo yako kwenye ukurasa wa   huduma zetu na pia ukishusha chini kabisa kuna sehemu ya kutuma ujumbe ambapo zilikuwa zinanifikia na nilishughulikia changamoto zao haraka iwezekanavyo. Kwa mwaka 2015 nategemea zaidi kupata maswali ya nini mtahitaji niwe nakiongelea au kitu ambacho haujakielewa kwenye baadhi ya machapisho au kwenye biashara yako. Nitaruhusu kupok...

Mabadiliko ya lazima kwa wafanyabiashara na wajasiriamali Tanzania

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa biashara unavyoenda hapa nchini basi utakuwa umeshagundua kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea ndani ya nchi hii, na sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni kutokana na Tanzania imekuwa ikifanya biashara kienyeji kwa muda mrefu na sasa imeonekana  katika ramani ya dunia wawekezaji na makampuni mengi ya kigeni yanakuja kufungua matawi na kuanzishwa hapa nchini hivyo serikali yetu imeona ni bora ianze kuwatengeneza wafanyabiashara mapema kabla haijajaa wawekezaji mfano: Serikali haikuwazoesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa EFD lakini imegundua kuna fedha nyingi zinapotea iwapo hawatatumia EFD ndio maana wakaamua kuwabana lakini kwa kuwa hawakuzoeshwa leo hii hadi Wahindi na Wachina ikiwa ni mgomo wa kufunga maduka nao wamo japokuwa kwao mtindo huu unatumika kitambo na biashara ni ushuru, lakini huku nao wako mstari wa mbele kufunga maduka. Baadhi ya mabadiliko haya yanatokea kwa kutangazwa na mengine hayatangazwi Mfano: Serikali iliona wimbi k...

Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo

Marketing kwa maana moja mimi huwa naiita ni zao la Branding kwenye biashara ambalo linatakiwa litoke liende kuitangaza brand iliyojitengeneza.Hapa nchini biashara nyingi zinafanyika kwa mazoea na watu wanafanya bila kuelewa au kuwa na maana halisi ya kitu wanachokifanya, utakuta mtu ameona kampuni fulani wamefanya kitu fulani kwa ajili ya bidhaa, biashara au huduma kwa ajili ya kampuni yao, basi na yeye pia atataka kubadilisha jina tu kwenye hicho kitu kutoka jina  la biashara alioiona hadi jina la biashara yake, ila vingine ataviaacha kama vya mwenzake kwa vile tu amependa jinsi kile kitu kilivyo. Na wengine hufanya hivyo kwa mifano na kujaribu . Leo nitaelezea kidogo vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kujitangaza au kufanya marketing,Tutaangalia vitu kama vitano(5) ambavyo unatakiwa kuviangalia kwenye biashara yako kabla ya kuanza kufanya marketing, vitu hivi mara zote huwa ni vitu vya kawaida na huonekana ni sio vya muhimu sana lakini nikupe siri ndugu yangu hakuna kitu a...

Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ujasiriamali na upungufu wa kazi kwa vijana.

Nchi yetu inaongozwa na sheria na moja kati ya sheria za nchi hii ni kila mtu ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake , hivyo na mimi nimeamua kutoa maoni yangu binafsi kuhusu hili suala la ujasiriamali hapa nchini , kwanza pongezi  kwa serikali kuona njia mbadala ya kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ni kufanya ujasiriamali , lakini nilikaa na kuangalia baadhi ya mambo nikagundua kuna mapungufu mengi na mara nyingi tumezoea kutaja matatizo ili uliemwambia atafute suruhisho. Hapo unakuwa unakosea kama yeye hakuliona tatizo unapompa tatizo tu bila suruhisho unampa kazi ya kufanya ambacho hakijui hebu fikiria nimekutengenezea gari lako na kukuletea mimi sio mtengenezaji wa kwanza inamaanisha ntarekebisha ili liwe kama awali wewe ndio unaetumia gari yako nikitengeneza isipofika unapohitaji ni lazima utaniambia bado ilikuwa anafanya hivi na hivi na hivi tofauti kabisa na huku kuna tatizo la maji kijijini watu wanaeleza tu tunashida ya maji tufikiriwe hata kidogo na sisi tunatembea...

Kwanini wajasiriamali wengi wanafeli?

Image
Kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa  wanahitaji kuwa wajasiriamali lakini asilimia kubwa wanakuwa ni wale ambao wanakuwa wamefeli mipango mikubwa au kuna kitu kimewasukuma ,vitu ambavyo unatakiwa usifanye kwa kudhani unatengeneza maisha utakuwa unapotea. Kuna kundi ambalo wao huanza ujasiriamali baada ya kuona umri unaenda au wanategemewa sasa na aidha famili a au kadahali Usifanye ujasiriamali kwa kuona umri umeenda upate kitu cha kujishikiza, hapo utafeli kumekuwa na watu wengi ambao hadi astaafu ndio anaanza ujasiriamali au baada ya kuona umri umeenda ndio anatafuta kitu cha kumpatia ujasiriamali hii ni mbaya na kufanikiwa kwake ni kugumu sana, ujasiriamali sio nyongeza ya ulichonacho ujasiriramali ni msingi wa ulichonacho kama hukutengeneza msingi mwanzo ujue hata uweke ukuta imara kiasi gani dhoruba ikija ni lazima nyumba itapata mtikisiko. Wapo wengine ambao wanafanya ujasiriamali  baada ya kukosa au kutuma sana maombi ya kazi ukifany...

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe  ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu  anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu  yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianz...

Nukuu za Chuma

Image