Posts

Jifunze kufanikiwa kwa kiwango ulichopo

Kila biashara hutegemea kufanikiwa katika eneo lake la ushindani lakini asilimia kubwa hufeli kwa vile hazitambui mafanikio yanahitaji vitu gani,chache ambazo hutambua uhitaji wa mafanikio hufanya ushindani na kujitengenezea nafasi katika soko, leo nitatoa siri 7 za vitu ambavyo vitakutengenezea mafanikio kwa sehemu na kiwango ulicho nacho kwa sasa:- 1.IBRAND BIASHARA YAKO. Branding sio neno geni na nimeshalitaja na kulielezea sana hivyo itengenezee muonekano wa tofauti katika soko lako, utofauti wako kwenye soko utakao kupa nafasi katika soko lako la ushindani na mafanikio ni matokeo ya ushindani. 2.UTAFITI Usifanye vitu kwa mihemko au kukurupuka  fanya utafiti wa kutosha kuhusu biashara yako  kuanzia vitu kama Eneo,Asili ya biashara, wateja wako,ushindani na aina zote za washindani, Mbinu shirikishi na vingine vingi, mafanikio hayawezi kuja iwapo hautajua uko katika kiwango gani na unakutana na ushindani aina gani,hilo unaweza kulielewa kwa kufanya utafiti tu hivyo t...

Jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia

Habari tena wanabranding, natumai mu wazima bukheri wa afya leo nimeona tukumbushane kidogo baadhi ya vitu ambavyo vitatusaidia wote kwa pamoja kuongeza masoko na kukuza uchumi wa taifa hili. Mada yetu leo inasema jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia siku baada ya siku. Utandawazi umebadilisha mambo mengi sana katika maisha ya mwanadamu na miongoni mwa vitu ambavyo viliguswa ni pamoja na sekta ya biashara ambapo kadri mambo na siku zinavyoenda nayo inaenda inabadilika hasa kwa huku kwetu nchi zinazoendelea. Teknolojia imekuja kurahisisha baadhi ya kazi na utendaji kazi wa eneo fulani miaka ya nyuma ilikuwa kama unahitaji kusajili kampuni yako ni lazima uende Brela ukaandike jina, utume barua, wakujibu ndio uanze kuomba usajili lakini sasa hivi kila kitu unakifanyia nyumbani kwa kutumia kompyuta yako tu. Tra nao vivyo hivyo ilikuwa ni lazima uende ofisi zao ili kulipa kodi lakini sasa unaweza kutuma hata kwa simu, hayo ni baadhi ya mabadiliko ya teknoloj...

Je! unajua maana ya Meme/Motto/Slogan katika biashara yako?

Watu wengi wamekuwa wanafanya vitu bila kutambua maana na kwanini, leo nitatoa dondoo kidogo kuhusu meme/Slogan/Motto. Hiki sio kitu kigeni lakini wengi tumwekuwa tukikifanyia mazoea leo pata darasa kidogo. Kila biashara inapofanyiwa branding lengo kuu liko kwa mteja na unapotaka kumpata mteja yoyote lazima uchanganye ahadi,ubora na picha. Ahadi hutolewa na Slogan au meme ya biashara, hivyo meme yako inamaana kubwa sana katika kuisimamisha biashara yako mfano. Katika magari Ukiwa unaendesha Marcedez Benz hata kama ni ya mwak 1921 bado slogan yake ni "expensive car" hata kama kiuhalisia sio kweli ila kwa vile brand yao ilitoa meme ya hivyo mteja anaweza kwenda kununua sio kwa sababu anaipenda Marcedez hapana ila tu ni kwa sababu its expensive car, gari aina ya BMW ni "comfortable car" nayo pia vivyo hivyo. Sasa basi nafikiri umepata picha ni kiasi gani meme inaweza kuathiri picha ya biashara yako aidha ukiifanya vibaya au vizuri. Chini hapa nakuwekea muongoz...

Maelezo kuhusu darasa la ujasiriamali.

Kama nilivyowaarifu hapo awali kutakuwa na darasa la branding na ujasiriamali kwa  watu wote wanaotegemea kuwa wafanyabiashara au wajasiriamali... nitatumia mtandao wa whatsapp kuendesha darasa hilo na litakuwa la mwezi mmoja kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupitia whatsapp Gharama za darasa itakuwa ni 25,000 kwa wiki 1 hivyo  kwa mwezi 1 ni sawa na 100,000 unaruhisiwa kulipia kila wiki . Faida za darasa hili ni 1.utajitambua mwenyewe uko kundi gani kati ya mjasiriamali au mfanyabiashara. 2.Utakuwa na uwezo wa kuona fursa na kupata wazo sahihi. 3.Kutambua aina za washindani katika biashara yako, na wapi ni hatari zaidi. 4.Pia utapokea sababu nyingi zinazofelisha wafanyabiashara wengi. 5.utapata muongozo wa kuanzisha na kusimamia biashara yako. 6.utapata ushauri binafsi 7.utapata muda wa kuuliza maswali yanayokutatiza. 8.Utapata muongozo wa Branding katika biashara. 9.Utapata nafasi ya kufahamiana na kubadilishana changamoto na wajasiriamali wengine. 10.Kila ...

Taarifa kwa Wasomaji wa blogu hii

Habari njema kwa wote mliokuwa mkifuatilia makala na matoleo yangu kuhusu ujasiriamali kupitia,blogu,kundi la whatsapp na  facebook.baada ya kuwa kimya kwa muda kidogo sasa nitaendelea tena kutoa makala na machapisho kupitia blogu yetu ya  www.elishachuma.blogspot.com  kuanzia mwezi wa pili  , na pia natarajia kuanzisha darasa la branding na ujasiriamali kwa wafanyakazi na wale wanaotegemea kuwa wafanyabiashara au wajasiriamali... nitatumia mtandao wa whatsapp kuendesha darasa hilo na litakuwa la mwezi mmoja kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupitia whatsapp number 0713603699. Branding ni kubwa sana kwa muonekano na kufikirika lakini ukiijua vizuri unaweza kubrand biashara yako katika hatua yoyote na ukafanikiwa,Karibu.

MABADILIKO YA MFUMO: TAHADHARI KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI

Habari za leo wana Branding, nimelazimika kurudia kupandisha uzi huu kutokana na hali ya mabadiliko ya kimfumo na kiuchumi inavyoendelea hapa nchini, nimepokea maswali mengi kuhusiana na ishu ya mabadiliko yanayoendelea serikalini na kimfumo pia,majibu yangu hayakuwa mbali na tahadhari hii niliyoitoa mwezi Oktoba 2013 lakini leo imeleta majibu kwa kuanza kuonekana hebu pitia na uyasome tena kwa makini kwa maana bado mabadiliko yanaendelea kutokea.... tuwemo. Taa ya hatari imeanza    kuwaka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Tanzania Asilimia kubwa ya wafanyabiashara, ( wakubwa na wadogo) wanafanya biashara Kienyeji na kikubahatisha wanafanya biashara kama mchezo wa bahati nasibu kupata Kukosa    lakini siku sio nyingi mambo na hali itabadilika na kubadili mfumo wote wa kibiashara Hapa Tanzania. Kwa kuanza kwa sasa watanzaia wengi wanapata hamasa na hamu ya kuwa wafanyabiashara Au wajasiriamali kwa inspiration kutoka nchi za nje, kutoka kwa w...

Aina za Brand

1.      Brand kama bidhaa Hufanya kazi ya ubora na thamani ya brand. Katika mkusanyiko wa matangazo ya bidhaa nyingi, mtumiaji huhitaji kujua jinsi ya kuchagua bidhaa moja juu ya nyingine, hivyo kwa kulinganisha udhania wake pale anapoamua kufanya hivyo huwa hana muda mwingi wa kulinganisha ,huamua kuchagua bidhaa ambayo inakidhi haja zake kutokana na brand. 2.      Brand kama mfumo/kampuni Hutengeneza muonekano chanya wa brand na huonyesha nyuma ya brand kuna mfumo Uwezo wa ushawishi wa kampuni hufanya bidhaa kuongeza thamani 3.      Brand kama mtu Hii hujishughulisha na uhusiano na wateja , hutengeneza kukutana kati ya mtu na brand Ni ngumu kuongeza soko kama hakuna mahusiano mazuri na wateja wako. 4.      Brand kama alama Hutoa muendelezo wa utambulisho wa brand Brand inayochukua akili yako hupata tabia , na brand inayochukua moyo wako hupata kujiapiza kwanz...