Posts

Jinsi ya kujitangaza na wapi pa kujitangaza

Utafutaji wa masoko umebadilija sana kipindi cha hivi karibuni kutoka mauzo mengi kwa ushawishi wa mdomo hadi kwenye kujitangaza kupitia mtandao. Asilimia kubwa ya wateja sasa hivi wanapatikana kwenye mtandao na asilimia kubwa ya biashara zinajitangaza kwenye mitandao,hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na upatikanaji wa taarifa nyingi muhimu kwa urahisi. Njia nyingine inayotumika ni kujitangaza kupitia mteja wako,biashara nyingi sasa hivi ziko kwenye utaratibu wa kutoa kamisheni kwa mteja atakae leta mteja mwingine,kwa sababu marketing ya mteja huwa ya uhakika na ya uzoefu hivyo humvuta mtu zaidi kutumia bidhaa au huduma. Hivyo ukiangalia njia zote mbili hapo juu ni kama zinaua soko la watu wa masoko badala yake linaongeza soko kwa watu wa teknolojia na habari hali imebadilika hii inakuja pia kama changamoto kwa sekta nyingine ya waliomo ndani ya kada ya kutafuta masoko na wanaofikiria kujiunga yafaa kuangalia zaidi mbele na dunia itahitaji nini zaidi kutoka kwako kwa muda gani...

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake. Hali ya mzunguko na mfumo wa biashara imebadilika sana hapa nchini na hii imechangiwa na kuongezeka kwa makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakiongeza chachu ya kuendelea kufanya zaidi ya pale wazawa wanapofanya, na tofauti kubwa ambayo inafanya kampuni nyingi na biashara nyingi za nje kufanikiwa ni Branding, asilimia kubwa ya hizo kampuni huingia nchini tayari zikiwa zimeshajibrand hivyo inakuwa rahisi kupata nafasi katika soko la ndani. Kinyume cha hapo asilimia kubwa ya biashara au kampuni zetu wazawa hazijafanya Branding ambayo ndio uti wa mgongo wa biashara, matokeo yake imekuwa hatuwezi kuuza ndani sababu hazina muonekano mzuri na hatuwezi kuuza nje sababu pia hazijafanyiwa branding nzuri. Baada ya serikali kuiona changamoto hiyo ikaanza kusisitiza wafanyabiashara kufanya branding vizuri( kuboresha  utengenezaji na upakiaji wa bidhaa uwe mzuri na wa kuvutia ili bidhaa zetu zipate nafasi hata katika soko la nje kwa wingi). Hivyo ...

Nembo yako inamaanisha nini?

Je wewe ni mfanya biashara au mjasiriamali au mfanyabiashara?umetengenezaje nembo yako? inakidhdi vigezo vya soko lako? Kwanza Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi. Kwanini biashara yako inahitaji nembo 1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako 2.Huonyesha muonekano unaotakiwa 3.hukuongezea hadhi 4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko 5.Kuwa na muonekano wa kuvutia 6.Hujipanga yenyewe kwa malengo flani ya soko. Vitu vya kuangalia unapotengeneza logo 1. Iwe ya kipekee 2. Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma 3. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea 4. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati) 5. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja y...

Mafanikio ya biashara yako na muonekano wake

Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana muonekano wako ambao hutengeneza uaminifu,heshima na kumvuta mteja, iwapo muonekano ukiwa tofauti na lengo mteja husita kufanya hivyo vilivyopo hapo juu, kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinachukuliwa cha kawaida katika kuipandisha na kuipa muonekano biashara yako ni fani ya Graphics design. fani hii kwa sasa imekuwa ni kama imeingiliwa kila anaetumia kompyuta basi anaweza kuwa graphics designer,hili limepelekea hadi sasa ubora wa muonekano na uhalisia wa kwanza wa biashara unapotea. Nguzo kuu ya Graphics design ni lazima dizaina awe anajua Branding,Maumbo,Mpangilio,fonts na rangi lakini sasa hivi vingi vinapuuzwa na kulifanya soko kuwa la kawaida,Je katika vitambulishi  vyako vyote viko sawa kulingana na maana ya rangi,maumbo,mpangilio na fonts kufuatana na uasili wa biashara yako? Makampuni makubwa husimamia zaidi suala la muonekano wao wanapokupa kazi wanatoa hadi na vipimo muonekano unaotakiwa na vipimo vya rangi ili usibadilishe mu...

Je unafahamu biashara yako inatakiwa iwe na muoneako gani ili iuze?

Serikali ya awamu ya 5 inapeleka mambo kasi na inathamisha katka mifumo tuliyoizoea na kutupeleka katika mifumo mipya, moja kati ya mabadiliko yanayoongelewa sana na yanayohitajika sana ni kukuza pato la taifa na kupandisha thamani ya pesa yetu hii inamaanisha ni kupunguza uagizaji na kuongeza uzalishaji kutokana na hilo serikali inashauri biashara ziongeze kujitangaza na kuuza nje ya mipaka ya Tanzania ili tuongeze kupokea malipo ya Usd kuliko sisi kulipa Usd.  Sasa basi moja kati ya kada zinazoangaliwa katika hili ni kada ya biashara ambapo inapokea urasmishaji na uboreshwaji wa mipango ya kimaendeleo kwa kasi sana hivyo biashara nyingi ambazo hazikuwa zimejipanga sawasawa kwenda na kasi yoyote nyingi zitakufa, lakini katika urasimishaji huu biashara haiongelei sana bidhaa ila inaongelea vitambulishi vya bidhaa, Katika mkutano wa wafanyabiashara kutoka India uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana rai yao ilikuwa ni kuboresha upakiaji na vifungashio vya bidhaa zetu hivyo kinachole ta...

Itambue kanuni kuu ya pesa

Kila kitu katika dunia hii kina kanuni aidha unaijua au hauijui, unaitambua au hauitambui leo nitaiongelea kanuni kubwa kabisa ya kwanza ya pesa. Kwanza kabisa nikubadilishe mawazo kuhusu upatikanaji na dhana ya mzunguko wa pesa. Kwanza ukubaliane na mimi kwanza kuhusu pesa kwamba, pesa uliyonayo mkononi,mfukoni,benki ama sehemu yoyote ile ambayo unaweza kuitoa kama unavyojiita mmiliki ile pesa sio ya kwako sababu kila pesa unayoishika tayari inasehemu au kazi ya kufanya na kama inasehemu au kazi ya kufanya inamaanisha inabidi ile pesa itoke mkononi mwako, hivyo wewe ni muwakilishi tu umeishika kwa muda huo ili uipeleke kwa mwingine, mfano Ukipewa 10,000 sasa hivi unajihisi kama wewe ni mmiliki wake lakini katika ulimwengu wa fedha wewe umekuwa daraja la mzunguko wake, hivyo kama ni daraja inabidi uipitishe ambapo lazima utaitoa na kumpa mtu mwingine hiyo pesa ambae hata yeye akiisha kuishika inakuwa sio yake tena inabidi akaitoe mfano umeenda kununua unga ukampa 10,000 atakurudishi...

Jinsi ya kutengeneza matokeo chanya kupitia business card yako.

Je unaitumiaje fursa ya kujitangaza kupitia Business card yako.japo bzcard ni kikaratasi kidogo kinaweza kukupa matokeo chanya zaidi ya vingine kwanza ni kidogo NA pia ni rahisi kukitunza tofauti na vingine hivyo ukikipa muonekano na maelezo sahihi kina matokeo chanya zaidi.lakini tuangalie hapa chini kwann tunakosea. kwanza Wengi wetu tumefanya business card kama karatasi ya namba tu,Ndio.Kwa nchi zilizoendelea bzcard imebeba namba tu labda na website.lakini kwa huku kwetu hali iko tofauti watu wengi hawakokaribu sana na matumizi ya mtandao zaidi wanatumia mtandao kupitia mitandao ya kijamii,hii inapunguza fursa ya kuitembelea tovuti yako. Pili asilimia kubwa ya watengenezaji na watengenezewaji huhisi bzcard ni bzcard tu haijalishi,lakini iko tofauti hata dizaini za bzcard zinatofautiana kulingana na kada tofauti tofauti,ukikosea kuitengeneza usitegemee kama atakaeiona atakufikiria kupitia kada yako.Mfano biashara ya chakula ikatengeneza bzcard kama za benki utaigusa ile bzcard unap...