Posts

Showing posts from 2017

Eneo sahihi la kuweka biashara yako.

Image
Tunapoelekea kuumaliza mwaka kila mtu anatakiwa kujichuja na kujitathmini ni sehemu gani ametelza ama amefanikisha kwa ufasaha na kuna wengine wanajitahidi mwaka usianze bila biashara zako kupata eneo la kuwekw sasa basi kumekuwa na changamoto kubwa kuhusiana na lipi ni eneo sahihi la kuiweka biashara yako,watu wamekuwa  na kasumba na kujifanyia hadi imefikia hatua hawajui athari zimeletwa na nini. Na hii inachangiwa mara nyingi na kufanya vitu bila kufuata weledi ama kuonana na washauri wa masuala hayo,mara nyingi biashara zinapoanza mwenye biashara hutafuta kuwa na sehemu tu ya kumfanya aonekane na yeye ana sehemu ya uelekezi (Physical  address) lakini inapokuja suala la kwanini amechukua eneo hilo huwa hana majibu ya moja kwa moja kama inamfaa ama haimfai kwa kulingana na biashara yake. Hili limekuwa tatizo kubwa sana na madhara yake yanaweza kuwa hayako moja kwa moja ila yanakutafuna mfano: ukiwa kwenye location sio unaweza kuwa unapata wateja wa mwisho na wa kw...
Image
Kwanini unatakiwa kumuweka ndani mtoto mchanga siku 40 baada ya kuzaliwa. Muda na wakati unatupa mkono sana katika kuijua kweli na hii inasababishwa na vitu vingi mabadiliko ya uchumi,hali ya hewa,mitindo ya maisha,kuiga na vichocheo vingi vinatufanya tunabadilisha ile kweli kuwa kawaida, leo nitaongelea suala la kwanini mtoto anapozaliwa anatakiwa kuwekwa ndani kwa siku 40 ni kitu ambacho tumekikuta tumekirithi lakini tunakiacha, Je vizazi vyetu ama kizazi chako cha 4 kitafahamu kama kulikuwa na kuweka 40 kama kuanzia kwako haujaweka 40?. Historia,zama na ukweli vinatupeleka mbali sana lakini hii dhana ya 40 haijatumika kwa mtoto tu vipo vingi leo tutaangalia kwanini mtoto. Sasa basi katika mwili wa binadamu kuna kitu kinaitwa Aura hiki hauwezi kukishika wala kukigusa ni kama tabaka lililopo juu ya mwili wako ambalo linakusaidia na kukukinga na nguvu za nje,mfano unaweza kutembea ukahisi mwili umesisimka ghafla tambua hapo aura yako imefanya kazi,ama umepima na unaumwa lakini...

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Image
Leo nimepata nafasi ya kuandika waraka huu kwa ajili ya kuwakumbusha kidogo wafanyabiashara wenzangu na wajasiriamali wenzangu kuhusu dhana moja ya muhimu sana iliyopo katikati ya mauzo na kujitangaza. Biashara nyingi sana sijajua kama ni kwa sababu ya kutokujua misingi ya biashara ama kutokuwa na uelewa wa kutosha na biashara zinafanya mambo kinyume na vile ambavyo inatakiwa na kujikuta zinatumia gharama kubwa kutengeneza mauzo kuliko ambavyo ingapaswa kuwa. Mara zote huwa nikipita na nikiwa kwenye semina huwa nawakaumbusha wafanyabiashara wenzangu na wajasiriamali kwamba siku zote usiwekeze kwenye kutafuta mauzo tu, kumbuka na kulijenga jina ama picha ya biashara, kuna faida nyingi sana za kujenga jina /picha katika kichwa cha mteja wako,lakini biashara nyingi hazifikirii sana kuhusu hilo bali wanawaza kuongeza mauzo tu. Siku zote mauzo ni mazuri lakini mauzo bila ya kuwa na jina ni gharama,nimeshakutana na wateja wengi sana wenye kutumia kauli hii " Mimi ninabi...

ENEO LA BIASHARA

Image
Kumekuwa na changamoto kubwa kuhusiana na lipi ni eneo sahihi la kuiweka biashara yako,watu wamekuwa  na kasumba na kujifanyia hadi imefikia hatua hawajui athari zimeletwa na nini. Na hii inachangiwa mara nyingi na kufanya vitu bila kufuata weledi ama kuonana na washauri wa masuala hayo,mara nyingi biashara zinapoanza mwenye biashara hutafuta kuwa na sehemu tu ya kumfanya aonekane na yeye ana sehemu ya uelekezi (Physical  address) lakini inapokuja suala la kwanini amechukua eneo hilo huwa hana majibu ya moja kwa moja kama inamfaa ama haimfai kwa kulingana na biashara yake. Hili limekuwa tatizo kubwa sana na madhara yake yanaweza kuwa hayako moja kwa moja ila yanakutafuna mfano: ukiwa kwenye location sio unaweza kuwa unapata wateja wa mwisho na wa kwanza wanaishia kwa mwenzako,hii itasababisha biashara kuwa na mauzo ya kawaida na kutokukua ,ikichelewa kukua inamaanisha malengo yatapishana na mipango ambapo kufeli kwake kunakuwa mlangoni lakini chanzo cha yote ni ku...

Jinsi ya kutengeneza Brand yako online

Image
Utengenezaji wa brand umebadilika sana kulinganisha   na hali ilivyokuwa zamani,na hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na ufanyikaji wa dunia kuwa kijiji hivyo hali hii imepelekea   hadi mfumo wa biashara nao kuhamia huko, mauzo yanayofanyika nje ya mitandao asilimia kubwa kwa sasa   ni matokeo ya ushawishi ama kujitangaza vizuri kupitia mitandao ya kijamii . Japokuwa tumekuwa tukiyaona na kuyashuhudia mabadiliko haya , bado hatujaweka mkazo mkubwa katika soko hili la kujitangaza online, mfano serikali inasema kuboresha vifungashio na muonekano wake hii inamaanisha lazima na soko la online( Mtandaoni) Uliangalie kama unataka biashara yako itoke sababu mtandao unafanya kazi dunia nzima na hicho ndicho kilichoufanya upate mwamko na kasi kubwa sababu unapokuwa kwenye mtandao unauwezo wa kujitangaza na dunia nzima ikakuona sasa ishu tuliyokuwa nayo ni kwamba kila kitu tunatengeneza chini ya kiwango lakini tunahitaji tuuze kwa kiwango cha juu. Mfano: Huwa m...

Wazo la 3

Vijana wengi na watu wengi wamekuwa na shida ya ajira sasa hivi ambapo imefikia hatua inabidi aajiriwe katika sekta isiyokuwa na weledi wake na wengine kukosa kabisa,wengine wanapesa za mitaji lakini hawana wazo bora la biashara waanzishe kitu gani ili kiwe na mafanikio kwao. Leo hii tutaenda kuangalia wazo jingine la biashara ambalo litawahusu sana akina mama na akina dada,katika mzunguko wa maisha wote tunatakiwa kutambua Mungu ni kiongozi na katika uumbaji wake hakuna alieumbwa kwa bahati mbaya na ndani ya kila mtu kuna kitu cha ziada ambacho Mungu amemuwekea kulingana na utashi wake..Leo nitawapa mbinu ya kujiajiri kwa madada ambao wanasema hawana ajira kabisa. Kuna baadhi ya kazi ambazo kama mdada ama mwanamke ukifanya kwa uhakika zinakutoa na hazihitaji chuo wala cheti ni kipaji na baraka tu baadhi ya kazi hizo ni pamoja na ususi,kutengeneza vitafunwa(bites),kufanya usafi na kadhalika,kama wewe unajijua unakitu unachoweza kukifanya kwa ufasaha kwa moyo wote bila kushurti...

Wazo la biashara 01

Asilimia 80% ya dawa tunazotumia mahospitalini zinatokana na miti,na asilimia 60 ya magonjwa tunayougua yanatokana na mtindo wa maisha, hivyo ukiwa kama mjasiriamali ama mfanyabiashara unatakiwa uone fursa hapo katikati ya kuugua na miti. Matunda yanatumika sana kama dawa, na chakula ni dawa ndio maana ukikikosea kinakuwa sumu mwilini sasa tupitie fursa hii,ikakufungue na kukupa maono mapya. FURSA: Unaweza  kuuza ujuzi  ama kuwa mshauri wa masuala ya chakula,matunda na miti. JINSI YA KUIFANYA: Kama mtumiaji wa mtandao anza kwa kutafuta na soma kwa makini    matumizi,faida,utengenezwaji,uhifadhi na mfumo wa mwanadamu unavyopokea na unatumia nini kwa matunda ambayo yanapatikana sana eneo lako ama yanayopatikana kwa urahisi ( Mfano kuchanganya tunda lenye ukali na lisilokuwa na ukali unaliua lile tunda lisilokuwa na ukali linakuwa pombe(Nanasi na ndizi).),fuatilia na chakula uandaaji,viungo,upishi na kadha wa kadha hakikisha unatambua kila aina ya chakula tunda ...

Tunza muda

Tunza sana muda wako, usiutumie muda wako kwa mazoea. Kwenye maisha pesa unaweza kuzitafuta na ukazipata lakini muda ukipita haujirudii tena kila sekunde, kama unafikiria kuwa na mafanikio hebu jiangalie unatumia muda kiasi gani kwa ajili ya uzalishaji katika siku yako. Anza upya badilika sasa...Jali muda #2017 #maishanihayahaya  wakubadilika ni wewe.

Tambua maana halisi ya fedha

Dhana ya  fedha haiko katika ile karatasi unayoishika yenye namba za thamani yake. Fedha yoyote unapoikea unaenda kuitumia hata kama sio moja kwa moja lakini wewe ni mwakilishi tu wa hilo karatasi ndio maana hazina mwenyewe unaishika wewe unaitoa anaishika mwimgine. Kama lile karatasi sio fedha basi fedha halisi iko wapi?...Fedha halisi iko kichwani mwako unapoifikiria na kuishughulikia hadi kuifanikisha hapo ndio unakuwa unafedha ila ukiisha kuishika tu wewe inakuwa sio ya kwako bali mtu mwingine ndio anakuwa anaiwazia na kuishughulikia aipate. Hivyo hakikisha kichwani mwako unatengeneza pesa nyingi bila kuchoka na jitahidi pia kuzishughulikia ukishazipata tu achana na zilizoingia sababu hata ufanyeje dhima ya pesa ni matumizi hivyo utaitumia tu.Ili kuwa katika sehemu nzuri kila siku tengeneza pesa akilini mwako. Ungana nami kwa dondoo na ushauri zaidi kuhusu ujasiriamali na biashara Jumatatu - Ijumaa saa 12:45ash - 1:00asubuhi (Maisha mseto) Redio Times fm 100.5 Kila Alhami...