Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.
Leo nimepata nafasi
ya kuandika waraka huu kwa ajili ya kuwakumbusha kidogo wafanyabiashara
wenzangu na wajasiriamali wenzangu kuhusu dhana moja ya muhimu sana iliyopo
katikati ya mauzo na kujitangaza.
Biashara nyingi sana
sijajua kama ni kwa sababu ya kutokujua misingi ya biashara ama kutokuwa na
uelewa wa kutosha na biashara zinafanya mambo kinyume na vile ambavyo inatakiwa
na kujikuta zinatumia gharama kubwa kutengeneza mauzo kuliko ambavyo ingapaswa
kuwa.
Mara zote huwa
nikipita na nikiwa kwenye semina huwa nawakaumbusha wafanyabiashara wenzangu na
wajasiriamali kwamba siku zote usiwekeze kwenye kutafuta mauzo tu, kumbuka na
kulijenga jina ama picha ya biashara, kuna faida nyingi sana za kujenga jina
/picha katika kichwa cha mteja wako,lakini biashara nyingi hazifikirii sana
kuhusu hilo bali wanawaza kuongeza mauzo tu.
Siku zote mauzo ni
mazuri lakini mauzo bila ya kuwa na jina ni gharama,nimeshakutana na wateja
wengi sana wenye kutumia kauli hii " Mimi ninabidhaa nzuri lakini mpinzani
wangu ananishinda sababu yeye anajina, watu wengi wanaenda dukani kuulizia bidhaa kwa jina lake,
mimi wanatumia kwa matumizi yake ambapo inaniwia vigumu kushindana nae"
Mfano huu na mingine
mingi ya kufanana na hii ni mifano hai ambayo ni kilio cha biashara nyingi sana, ambapo hujikuta zinatumia gharama kubwa kujitangaza ama kuitangaza bidhaa bila
kujenga jina.Mauzo bila ya kuwa na jina (Brand) ni gharama sana.
Unapouza ama
unapotangaza biashara yako ili inunuliwe peke yake maana yake ni kwamba utakuwa
unaitangaza kila siku ili upate wateja, na pia hautafahamika kwa wateja wako
zaidi ya bidhaa tu, lakini ukiwa unajenga jina unakuwa na nafasi kubwa ya kuwa
mshindani sokoni hata kipindi ambapo haujaweka nguvu nyingi katika kujitangaza
jina lako litakupa nafasi kwenye soko lako.
Faida za jina ni
pamoja na, kuwa na uwezo wa kuwa mshindani sokoni,kuwa na uwezo wa kupanga
bei,kuwa na uwezo wa kuigwa ,kukaa ndani ya vichwa vya watu,kuwekwa kumbukumbu
muda wote ambao unajitangaza hata ule ambao haujitangazi.Makampuni makubwa
yanatumia muda mwingi kutengeneza picha ndani ya kichwa cha mteja wake, kuliko
mauzo kwa kuwa yanaamini kuwa mteja akishapata picha na ikatunzwa ndani ya
kichwa chake, yatakuwa na kazi ya kuwakumbusha tu sio tena kujieleza kama ukiwa
hujajenga picha.
Umeshawahi kujiuliza
kwanini matangazo mengi barabarani huwa hayana maelezo mengi tofauti na picha
ama nembo za kampuni husika?, wakati ni gharama kuyaweka hapo barabarani? Hiyo
nafasi ungeipata wewe ungesema tena barabarani ujaze bidhaa zako zote na uandike
kila unachofikiria ili kuhakikisha unatangaza kila kitu kupitia hapo.Lakini ni
kwanini basi haiko hivyo?
Maana ya kufanya
hivyo ni kwa sababu wanahitaji kumkumbusha mteja kuhusu nembo ama picha yao tu
na mteja atakumbuka bidhaa zao, mathalani tufanye ni mtandao wa simu, ukiona
tangazo barabarani kwenye zile nguzo za taa limechorwa nembo ama picha tu wewe
kichwani kwako zitakuja huduma zote za kampuni hiyo…( Kurusha fedha,Kutuma
sms,kutumia data, kumtafuta mtu wa mtandao huo,kumpigia mtu wa mtandao huo,
yaani utakumbuka kila kitu ambacho kinahusiana na mtandao huo ) lakini kama
wangeandika mfano ni promosheni ya vocha utakumbuka kuhusu vocha tu na
kulinganisha na mtandao mwingine basi ukawa umemaliza kuwafikiria.Lakini yote
hayo yanatengenezwa na kujenga picha/jina ndani ya kichwa cha mteja husika.
Sasa basi biashara
nyingi zinafungwa kwa sababu gharama za kujitangaza ni kubwa sana kuliko mauzo
ama zinachukua nafasi kubwa ya faida, hivyo inakuja kuingilia na matumizi, biashara inajikuta inafeli kuendelea na kufungwa,usitumie nguvu nyingi sana kwa ajili ya kupata mauzo tengeneza mauzo
yako kupitia kujulikana kwako na jina lako,itapunguza sana kiwango cha gharama
ya kujitangaza kwa nguvu kama mwanzo.Lakini tatizo kubwa la wafanyabiashara
huwa wanataka kila tangazo liwe ni la kuleta mauzo bila kujenga jina .Na hatua
ya kujenga jina sio hatua ya siku ama mwezi hivyo wengi huona kama wanapata wateja sio shida hivyo kuendelea tu ila muda wa kutumia jina ama brand ukifika
wanajikuta hawana tena uwezo wa kufanya hivyo ,biashara inafungwa kwa sababu
inategemea mauzo peke yake.
Hivyo badilisha
namna ya kujitangaza kwako,namna ya kuhudumia wateja wako na hata namna ya
kutengeneza mpango chapa wako,ijenge brand yako ikujenge.ila tambua kujenga
brand sio shughuli ya siku 1 ama 10 inachukua muda lakini matokeo yake ni
makubwa.kwa biashara yenye malengo ambayo inatakiwa kukua na kusimama kwa muda mrefu ni lazima itumie mbinu za kuwepo sokoni muda mrefu.
Amka leo usiendelee
kuiweka biashara yako katika hatari ya kufeli sababu ya kufikiria mauzo peke
yake,tengeneza jina huku unajenga mauzo mwisho utakuja kuona faida yake
biashara inayodumu sokoni ni ile
inayojijenga sio inayojitangaza tu,tengeneza brand ya biashara yako leo Ili
upate nafasi sokoni .
Mauzo ni mazuri
lakini mauzo bila kujenga jina ni gharama sana,na hiyo gharama ni ngumu
kuisimamia kwa biashara zinazoanza na zinazoendelea kukua.
Da ii post nimechelewa kuiona labda nlikuw mdogo sema jamaa umetoa elim ambayo inaishi kwa kizazi hiki nimeelewa napafanyia kazi
ReplyDelete1xbet | 1xbet | Bet with a Bonus - RMC | Riders Casino
ReplyDelete1XBet allows you to 출장마사지 bet on 1xbet korean any favourite horse https://septcasino.com/review/merit-casino/ races or any other herzamanindir.com/ sporting event. ✓ Get up casinosites.one to £300 + 200 Free Spins No Deposit
Best
ReplyDeleteUko vizuri sana kaka mkubwa
ReplyDelete