Baadhi ya sehemu ambapo watu wengi wanafeli na kunyanyuka kwao kunakuwa kugumu ni kati ya muumganiko wa kile anachokiwaza na uhalisia,na hii inachangiwa sana na kutengeneza mipango isiyokuwa na uhalisia wa maisha ama mzunguko wako wa maisha yako ya kila siku.Usitegemee kuja kufanikiwa kwa mpango ambao utaubadilisha zaidi ya asilimia 40 ya maisha yako ya kila siku,hakikisha mpango wako unazingatia uhalisia wa mzunguko wa maisha na uwezo wa kuufanya uwe hai.Simamia kuunganishwa kwake. Kitu kingine kinachowa rudisha nyuma watu wengi ni kuishi maisha ya wenzie,hata umempata roll model wako kamwe usitake kuishi kama anavyoishi yeye sasa hivi ukitaka uwe kama roll model wako anza kwanza kufatilia alifanya nini kabla ya kuwa kama alivyo usimuige kama alivyo sasa ila mfatishe alivyofanya hadi akawa kama alivyo sasa hivi.Kwenye akili unabeba ndoto kubwa ili uendane na roll model wako matokeo yake unafeli nakumfaidisha yeye. Pia kingine na kikubwa zaidi unatakiwa kujitambua ili maw...
Posts
Showing posts from 2018
Matumizi ya muda
- Get link
- X
- Other Apps
Muda ndio chanzo cha mafanikio yako, na jambo lolote ukitaka lifanikiwe lifanye kwa kuzingatia wakati,watu wengi wanashindwa kufikia malengo sababu hawauzingatii muda wao,wanaishi kwa kuzingatia pesa na sio muda wa kutafuta pesa matokeo yake anakuja kupata pesa lakini muda umemuacha ama hata kuzikosa.Matumizi ya muda wako ni ya muhimu sana sababu siku zote muda ndio unaotengeneza pesa hivyo usipoujali muda inamaana unapoteza pesa.KUWA MWANGALIFU PANGILIA MATUMIZI YA MUDA WAKO KUANZIA DAKIKA HADI MWAKA NA USIMAMIE MATUMIZI YAKE.UTAFANIKIWA.
KANUNI YA KUFANIKIWA NA FEDHA
- Get link
- X
- Other Apps
Haya maneno yamezoeleka kutumika na yamekuwa ya kawaida sana japo yanamsingi mkubwa katika mafanikio yetu ya kila siku,kuna baadhi ya mambo tumeyageuza juu chini ambapo kwa sasa yanatusumbua sana kiimani,kiuchumi na hata kielimu,hebu angalia hiyo formula hapo juu,iko hivyo katika maisha yako? Nitairudia tena kisha nitaidadafua ili uelewe na kisha uone unakosea ama tunakosea wapi katika kutengeneza pesa na mafanikio kwa ujumla formula inasema FEDHA = SHUKRANI,SHUKRANI = BARAKA. Kwahiyo BARAKA = FEDHA Kiuhalisia na mtindo wa maisha tuliochagua aidha kwa kurithi ama kuamua ni kwamba formula iko kinyume FEDHA = BARAKA, BARAKA zinatoa SHUKRANI, ndio maana mafanikio ya watu wengi yanakwama kwa sababu ya kugeuza kanuni ya mafanikio unakuwa unajali zaidi kupata pesa kuliko baraka ambazo ndio chanzo cha fedha zenyewe haya tuipitie kanuni hapa chini utakubaliana na mimi. FEDHA = SHUKRANI ( Malipo ya kazi ama kitu chochote unachokifanya ni shukrani ya kile ulichokifanya wala sio w...
NENO LA LEO : USIOGOPE
- Get link
- X
- Other Apps
Usiogope usinung'unie aliekuchagua bado hajachoka haijalishi uko kwenye hali ama hatua gani amesema yuko pamoja nawe,usijione peke yako katika hali yako lakini la msingi ni USIOGOPE KWA SABABU YA HAO.jitathmini leo kinachokuogopesha na kukurudisha nyuma kina nguvu kuliko neno lililosema Usiogope. Haijalishi kikwazo chako usiogope songa mbele,Bwana yu pamoja nawe.AMKA simama endelea na safari ushindi ni wako ila tu usikate tamaa na kurudi nyuma.Uwe na Jumapili njema.
UNAWEZAJE KUKUZA BRAND YAKO.
- Get link
- X
- Other Apps
Mjali mteja wako Tengeneza nafasi ndani ya kichwa cha mteja wako Weka muhuri wa moto kwa mteja Kuwa karibu sana na wateja wako wakubwa Kutengeneza utambulisho wa kampuni Kutoa msaada Kuwekeza Toa taarifa bure Ongeza thamani ya biashara Iweke brand yako nje ya boksi Fanya mawasiliano ya mteja mmoja mmoja Fanya udhamini wa maonyesho. Vyombo vya habari Vyombo vya ndani Kutengeneza vipindi vya mahojiano Udhamini Maandishi ya kushukuru Ofa maalum Sehemu za ushindani Blog,Website, Offline. Tambua jumuiya Tambua wateja kama ni biashara mpya tengeneza Nembo . Kuna nembo aina 3 Rangi ni muhimu Aina ya soko Nembo haitakiwi kuwa bize Nembo huleta matokeo chanya iwapo itatumika vizuri Nembo ni sehemu kwenye picha ya kampuni. Utambuzi wa brand Unatakiwa uanze ndani ya biashara kisha ndio ije kwa wateja na wapinzani Muonekano wa juu juu wa biashara yako, ona unaona nini? Ni nini...