KANUNI YA KUFANIKIWA NA FEDHA
Haya maneno yamezoeleka kutumika na yamekuwa ya kawaida sana japo yanamsingi mkubwa katika mafanikio yetu ya kila siku,kuna baadhi ya mambo tumeyageuza juu chini ambapo kwa sasa yanatusumbua sana kiimani,kiuchumi na hata kielimu,hebu angalia hiyo formula hapo juu,iko hivyo katika maisha yako? Nitairudia tena kisha nitaidadafua ili uelewe na kisha uone unakosea ama tunakosea wapi katika kutengeneza pesa na mafanikio kwa ujumla formula inasema FEDHA = SHUKRANI,SHUKRANI = BARAKA. Kwahiyo BARAKA = FEDHA Kiuhalisia na mtindo wa maisha tuliochagua aidha kwa kurithi ama kuamua ni kwamba formula iko kinyume FEDHA = BARAKA, BARAKA zinatoa SHUKRANI, ndio maana mafanikio ya watu wengi yanakwama kwa sababu ya kugeuza kanuni ya mafanikio unakuwa unajali zaidi kupata pesa kuliko baraka ambazo ndio chanzo cha fedha zenyewe haya tuipitie kanuni hapa chini utakubaliana na mimi. FEDHA = SHUKRANI ( Malipo ya kazi ama kitu chochote unachokifanya ni shukrani ya kile ulichokifanya wala sio w...