Posts

Hali za kimaisha za vijana zisitumike kama mtaji wa kisiasa kwa vyama na wanasiasa.

Image
Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa wewe ambae umeendelea kunitumia ujumbe mfupi ,kunipigia simu na kunitumia barua pepe kwa ajili ya shughuli hii,siwezi kuwataja wote kwa majina lakini ninautambua mchango wenu bila kusahau wapenzi wa blogu hii ambao huendelea kutembelea blogu hii hata kama sijaweka uzi upya niwashukuru kwa namna ya kipekee kabisa. Baada ya kupita kimya kidogo cha kutokuwa na uzi nimeonelea kwanza leo tuzungumze kidogo na vijana wa taifa hili maana hakuna familia isiyokuwa na kijana au vijana katika nchi hii, hata kama hatakuwepo kijana basi kutakuwa na kijana mtarajiwa.Tuko katika kipindi cha uchaguzi hivi sasa na watu wengi wanajitahidi kupata nafasi au sehemu ya kujishikiza kwa kipindi hichi ili angalau na wao wapate japo kidogo kitu katika mzunguko huu wa kampeni na mchakato wa uchaguzi kama mlivyoona kwa sasa kuna kampeni na zoezi la uandikishaji wapiga kura ambapo zinatumika mashine za BVR asilimia kubwa ya waandikishaji...

Vitu vinavyofanya Brand ya kawaida kuwa brand kubwa na bora

Vitu vinavyofanya brand ya kawaida kuwa brand kubwa na bora WAZO Nyuma ya kila brand nzuri lazima kuna mawazo mazuri ambayo hutumika kukamata hisia za wateja na mawazo kwa kuhisi shida zao zitamalizwa hapo UPEKEE Inatakiwa ikutofautishe na brand nyingine kwenye sekta hiyo MVUTO Brand inatakiwa kuwa na mvuto kwa watu kuanzia nembo zake hadi kutamkwa kwake.Brand bora huhakikisha wateja wake wanaelewa ahadi zake na kuvutiwa nazo. UWAJIBIKAJI Wateja wanahitaji   kuamini na kuziona ahadi zilizowekwa zinatendeka kama ilivyopangwa na zinawafikia kwa muda sahihi. UIMARA Wateja huhitaji kuhudumiwa na brand iliyo imara ambayo haitalegalega kipindi watakoihitaji. MAWAZO YA MUDA MREFU Mawazo ya muda mrefu huisaidia brand kujiimarisha na kujipanga vizuri kw a ajili ya kufahamika na kuwatembelea wateja wake duniani UHALISIA Brand bora inatakiwa kuonyesha uhalisia , na inatakiwa kufikia kile ambacho watu wanataka , inafanya kazi jinsi ambavyo waan...

Kwanini usiache kuendelea kujitangaza na kutafuta masoko hata kama biashara yako inafanikiwa.

Nimekuwa nikiulizwa hili swali mara nyingi sana kuhusu mafanikio ya biashara na muendelezo wa matangazo, na asilimia kubwa ya wanaouliza swali hili ni wale ambao biashara zao zimefanikiwa au malengo waliyokuwa wameyaweka yamefikia au yamekaribia sana. Mara zote jibu langu huwa ni moja tu. Msingi wa biashara yako uko kwenye kujitangaza hivyo ukisimama kujitangaza basi na biashara itasimama kuingiza mauzo. Leo nimeona niweke hapa chini baadhi ya sababu ambazo zinakufanya kama mfanyabiashara au mjasiriamali usiache kuendelea kujitangaza. 1. Ushindani haukomi katika ulimwengu wa biashara mafanikio au kushindwa kunaletwa na ushindani,biashara isiyokuwa na ushindani haiwezi kujijua kama inashinda au inafeli sababu hakutakuwa na mwingine wa kuikumbusha kufanya ambavyo inatakiwa kufanya. Hivyo kama biashara yako iko sokoni na inafanya kazi kujitangaza hakukomi sababu mshindani wako kila siku anafikiria njia na namna ya kukushinda kibisahara mteja aliekuja kwako leo kesho awe ni mteja wake...

Kazi na Aina za Branding

Karibu katika muendelezo wa somo la Branding na leo nimekuletea kazi na  aina za Branding katika maisha ya biashara zetu, watu wanafikiri Branding ni kitu kigeni katika ulimwengu wa biashara La Hasha! Branding sio kitu kigeni na kila mtu kila siku anafanya Branding.Hapa chini ni baadhi tu ya kazi za Branding katika biashara yako. Branding ndio muongozo au chanzo cha mauzo yako, iwapo utajibrand vibaya mauzo yako yatakuwa mabaya na iwapo utajibrand vizuri mauzo yako yatakuwa mazuri,Kazi ya masoko ni kuipeleka Branding nje ya ofisi ambapo kama ahadi na muonekano ulioweka kwenye brand yako utakuwa mzuri na wenye kumvutia mteja basi huyo atakuwa mteja wako ila ikiwa tofauti na hapo utakuwa umemkosa mteja. Kazi za Branding Brand   hutambulisha muonekano ,ubora   wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)   hazijulikani   na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu Brand hutofautisha bidhaa na hufanya ...

Muongozo wa kuanzisha biashara

Biashara imekuwa ni ndoto ya watu wengi wake kwa waume,vijana kwa wazee na katika mizunguko zunguko yangu nikaona leo ngoja niongelee hili suala ambalo linabeba ndoto za watu wengi,mafanikio na ajira za watu wengi. Kwanza kitu cha kwanza ambacho unatakiwa ukitambue ni kwamba mafanikio au kufeli kwa biashara yako kunategemeana sana na vitu vifuatavyo Ujuzi wa kazi Hamasa Nguvu  Maono na Uwezo wa mfanyabiashara au mjasiriamali huyo. Hivyo kwa kuanza tu leo nitakupa vitu vitakavyokupeleka katika mafanikio ya biashara yako tangu inapoanza hadi ukuaji wake. Tambua uwezo wako unapoamua kuanzisha biashara shirikisha na upendo ulionao kwenye hiyo kazi na mvuto ulionao kweye biashara hiyo Fikiria kupitia biashara yako unaisaidia dunia Siku zote fikiria kuhusu mteja wako sababu biashara yako ni kuhusu wateja wako Tambua kwamba biashara ni utatuzi wa matatizo ya wateja Hakikisha unambinu zilizokamilika Hayo ni mambo makuu ambayo ukiyatambua unapoanzisha biashara basi...

Umuhimu wa Broshua katika biashara yako

Broshua haina tofauti sana na Kipeperushi lakini yenyewe inakuwa imedizainiwa na kuprintiwa pande zote na kukunjwa ,lakini kipeperushi chenyewe  hakina kukunjwa na huprintiwa pande moja tu. Broshua hazitolewi kama kipeperushi mara nyingi broshua hugawiwa na mtu wa masoko baada ya kuona mteja amevutiwa na kitu fulani au anahitaji maelezo zaidi ya kitu ambacho maelezo ya kina yapo kwenye broshua hiyo au amevutiwa na kitu fulani, Broshua ni lazima iwe ni nzuri na nadhifu. Sababu za kutoa Broshua ni pamoja na Kufuatilia maelezo zaidi kuhusu mawasiliano ya mauzo Kutoa maelezo ya kina na mengi zaidi kuhusiana na biashara,bidhaa au promosheni Kupata muitikio wa mteja mtarajiwa kwa kuonyesha uwezo,gharama na mategemeo Watu wengi wamekuwa wanaacha kujitangaza au kutengeneza vitu vya kujitangaza kwa vile tu pale mauzo yanapoongezeka ni makosa kusimamisha promosheni kwa ajili tu unapata faida inatakiwa kila siku kuwe na promosheni inayoendelea ndani ya biashara yako na ...

Umuhimu na maana ya Kipeperushi(Flyer) katika biashara yako.

Image
                               Kipeperushi ni karatasi isiyokunjwa iliyodizainiwa vizuri mahsusi kwa ajili  ya kukutangaza,na inatumika kuweka umakini kuhusu tukio,huduma,bidhaa au wazo . Kipeperushi kama kinavyoitwa hutumika kupeperusha habari au tangazo lako na kipeperushi mara nyingi hubeba ujumbe rahisi na mwepesi kufika kwa walengwa,kipeperushi hutumika sana kwenye halaiki ya watu wengi, Vipeperushi havina gharama kubwa na pia ni njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Aina hii ya kujitangaza kupitia kipeperushi huitwa tupa mbali, kwa sababu mara nyingi mtu anaepewa kipeperushi mara nyingi anakuwa kwenye mwendo ambapo akisoma anapomaliza wengi  wao huvitupa kwa kuwa ameshakisoma ambapo sehemu atakapo kitupa yeye pia kuna mwingine atakiokota ili aone ni tangazo la nini na yeye atafanya vivyo hiyo akimaliza kusoma hivyo habari inawafikia wengi kwa mtindo wa...