Umuhimu na maana ya Kipeperushi(Flyer) katika biashara yako.

                             
Kipeperushi ni karatasi isiyokunjwa iliyodizainiwa vizuri mahsusi kwa ajili  ya kukutangaza,na inatumika kuweka umakini kuhusu tukio,huduma,bidhaa au wazo .

Kipeperushi kama kinavyoitwa hutumika kupeperusha habari au tangazo lako na kipeperushi mara nyingi hubeba ujumbe rahisi na mwepesi kufika kwa walengwa,kipeperushi hutumika sana kwenye halaiki ya watu wengi, Vipeperushi havina gharama kubwa na pia ni njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja.

Aina hii ya kujitangaza kupitia kipeperushi huitwa tupa mbali, kwa sababu mara nyingi mtu anaepewa kipeperushi mara nyingi anakuwa kwenye mwendo ambapo akisoma anapomaliza wengi  wao huvitupa kwa kuwa ameshakisoma ambapo sehemu atakapo kitupa yeye pia kuna mwingine atakiokota ili aone ni tangazo la nini na yeye atafanya vivyo hiyo akimaliza kusoma hivyo habari inawafikia wengi kwa mtindo wa kupeperusha.

Mara nyingi vipeperushi hutumika  kwa ajili ya

  1. Matangazo ya tukio sana sana Tamasha na kufungua club
  1. Maelezo ya bidhaa ,kama uwezo wa bidhaa mpya na ubora

Watu wengi hufikiria kuwa kwa vile vipeperushi mara nyingi hutupwa basi itakuwa ni hasara kwa wao kutengeneza kitu ambacho kitatupwa badala ya kutunzwa, lakini ukitengeneza vipeperushi unakuwa unaitengenezea biashara yako uwezo mzuri wa kuonekana na nafasi katika ushindani, usifikirie kuacha kufanya promosheni ya biashara yako kwa vile tu unaona unapata faida biashara ni matangazo na ushindani hivyo usisitishe hata mara moja

Chapisho lijalo nitaelezea kwanini biashara yako inatakiwa iwe na Broshua


Bado mnakaribishwa kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko lazima.



Pia karibu utangaze nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia blogu hii maelezo zaidi kuhusu kutangaza piga simu nama 0713603699.

Comments

  1. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango